Home » » MAMA JANETH MAGUFULI AAHIDI KUENDELEA KUSAIDIA KAMBI ZA WAZEE NA WATU WENYE ULEMAVU NCHINI.

MAMA JANETH MAGUFULI AAHIDI KUENDELEA KUSAIDIA KAMBI ZA WAZEE NA WATU WENYE ULEMAVU NCHINI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Wananchi wa Kijiji cha Nandanga Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi wakimlaki Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli aliwapowasili eneo hilo kwa ajili ya kutoa Msaada wa Vyakula, Mafuta pamoja na Dawa kwa ajili ya Kambi ya Wazee ya iliyopo katika kijiji hicho.

Mratibu wa kambi ya Kulea wazee na watu wenye ulemavu ya Nandanga Bw. Agnerus Chiamba akimpa maelezo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli kuhusu nyumba za malazi katika kambi hiyo, aliwapowasili eneo hilo kwa ajili ya kutoa Msaada wa Vyakula, Mafuta pamoja na Dawa.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi akimuonesha Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli nyumba za malazi katika Kambi ya Wazee na watu wenye ulemavu ya Nandanga iliyopo katika kijiji hicho aliwapowasili eneo hilo kwa ajili ya kutoa Msaada wa Vyakula, Mafuta pamoja na Dawa.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akifungua kitambaa kuashiria kuwekwa jiwe la msingi la zahanati ya kijiji cha Nandanga itakayorahisisha upatikanaji wa huduma ya afya kwa wakazi wa eneo hilo waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo.
Baadhi ya Vitu vilivyotolewa kwa ajili msaada katika kambi ya kulea Wazee na watu wenye ulemavu ya Nandanga.

Jengo la Zahanati ya Nandanga lililozinduliwa na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli

Mratibu wa kambi ya Kulea wazee na watu wenye ulemavu ya Nandangwa Bw. Agnerus Chiamba akimkabidhi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli taarifa ya kambi ya Kulea Wazee ya Nandanga

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli wakati wa hafla ya utoaji misaada katika kambi ya kulea wazee ya Nandanga iliyopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi akimkabidhi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi akiwaeleza Jambo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli (Katikati) na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mama Mary Majaliwa.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mama Mary Majaliwa Wakicheza Ngoma na kikundi cha Vijana wakati wa hafla ya utoaji misaada katika kambi ya kulea wazee ya Nandanga iliyopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.

Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mama Mary Majaliwa akiongea na wananchi wa Kijiji cha Nandanga na kumshukuru Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli kwa kutoa msaada katika kambi ya Wazee na watu wenye ulemavu iliyopo katika kijiji hicho.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli(kushoto) akikabidhi misaada kwa wawakilishi wa kambi ya kulea wazee ya Nandanga iliyopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi, Katikati ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mama Mary Majaliwa.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na wananchi wa Kijiji cha Nandanga kilichopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi na kuahidi kuendelea kusaidia kambi za wazee na watu wenye ulemavu wa ukoma ambapo mpaka sasa meshatoa msaada katika kambi 4 katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Lindi na Mtwara yenye thamani ya Takribani shilingi 250.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akipokea zawadi kutoka wawakilishi wa wananchi na wazee wa kijiji cha Nandanga kilichopo Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na baadhi ya watoto waliofika katika hafla ya utoaji misaada katika kambi ya kulea wazee ya Nandanga iliyopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiagana na wananchi wa Kijiji cha Nandanga kilichopo Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi baada ya kutoa msaada katika kambi ya kulea wazee ya Nandanga iliyopo eneo hilo.
PICHA NA HASSAN SILAYO

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa