Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Chirangalile kata ya Makanjiro Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi Mohammed Rashidi Abdallah akitoa maelezo kwa mwombaji nafasi za Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kupitia Mpango Jumuishi Viola Ngonyani
Na. Elimu ya Afya kwa Umma.
Vijana
katika maeneo mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
Mkoani Lindi weendelea kuwasilisha maombi ya kuwania nafasi za Wahudumu
wa Afya Ngazi ya Jamii kupitia Mpango Jumuishi.
Akizungumza
Ofisini kwake wakati wa kupokea maombi Afisa Mtendaji wa Kijiji cha
Chirangalile kata ya Makanjiro Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani
Lindi Mohammed Rashidi Abdallah amesema katika kijiji chake tayari
wameshapokea maombi kwa asilimia 85%.
"Tunashukuru
zoezi la kupokea maombi linaendelea vizuri katika kijiji chetu ambapo
maombi yamefikia asilimia 85% hivyo niwasihi wakazi wa eneo hili hasa
vijana waliomaliza kidato cha nne wachangamkie fursa hii ambao wataenda
kusaidia katika eneo la afya ngazi ya jamii"amesema.
Naye
Viola Ngonyani mmoja wa vijana waliowasilisha maombi ya kuwania nafasi
ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii amesema ameamua kuwania nafasi hiyo
ili kuweza kushirikiana na Serikali kutoa huduma za afya karibu zaidi
na Wananchi.
Kwa Upande
wake Afisa kutoka Wizara ya Afya, Idara ya Kinga, Sehemu ya Elimu ya
Afya kwa Umma, Mpango wa Taifa wa Huduma za Afya Ngazi ya Jamii Orsolina
Tolage ametumia nafasi kujibu Maswali mbalimbali yanayoulizwa na vijana
huku akisisitiza kuwa kila kijana mwenye vigezo husika ana haki ya
kuwania nafasi hiyo muhimu.
0 comments:
Post a Comment