Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mtwara ndugu Mohamed Sinani akikabidhi
picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa Mama Salma Kikwete na picha
ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mheshimiwa Abeid Aman Karume kuashiria
muendelezo wa mbio za uzalendo za pikipiki kusherehekea miaka 50 ya
Mungano wa Tanganyika na Zanzibar hapo.
Mwenyekiti
wa CCM wa Mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Said Sinani (mwenye kofia)
akifuatana na viongozi wenzake wa Chama Cha Mapinduzi na Umoja wa Vijana
kwenda kukabidhi mbio za pikipiki kwa uongozi wa Mkoa wa Lindi kwenye
Kijiji cha Madangwa jana.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa
Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsikiliza kwa makini
mtoto Idd Omar kutoka katika Kijiji cha Madangwa , kata ya Sudi huko
Lindi Vijijini. Mama Salma alifika kijijini hapo kwa ajili ya kupokea
mbio za uzalendo za pikipiki zilizoandaliwa na Umoja wa Vijana, (UVCCM)
kitaifa zikitokea Mkoa wa Mtwara.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaelekeza baadhi ya wanafunzi wa Shule ya
Msingi ya Madangwa namna ya kushika mfagio ili usiweze kuleta madhara
kwa watoto waliobeba na hata wengine na pia ni njia bora ya kulinda afya
zao kwani wakishika upande unaotumika kufagia wanaweza kupata magonjwa
ya kuambukizwa.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaelekeza baadhi ya wanafunzi wa Shule ya
Msingi ya Madangwa namna ya kushika mfagio ili usiweze kuleta madhara
kwa watoto waliobeba na hata wengine na pia ni njia bora ya kulinda afya
zao kwani wakishika upande unaotumika kufagia wanaweza kupata magonjwa
ya kuambukizwa.
Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mtwara ndugu Mohamed Sinani akikabidhi
picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Lindi Mzee Ali Mtopa na picha ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mheshimiwa
Abeid Aman Karume kwa Mama Salma Kikwete kuashiria muendelezo wa mbio za
uzalendo za pikipiki kusherehekea miaka 50 ya Mungano wa Tanganyika na
Zanzibar. KWA MATUKIO ZAID KATIKA PICHA BOFYA READ MORE
Makabidhiano rasmi yakiendelea huku mamia ya wananchi waliofurika kushuhudia wakishangilia.
Baadhi ya Viongozi
wa juu wa Chama Cha Mapinduzi kutoka Mikoa ya Lindi na Mtwara wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiana mbio za pikipiki
kusherehekea miaka 50 ya Mungano.
Bwana
Salum Musa Mtungulu mkazi wa Kijiji cha Madangwa alitumia fursa hiyo ya
makabidhiano ya mbio za pikipiki kurejea Chama Cha Mapinduzi akitokea
Chama Cha NCCR- Mageuzi. Katika picha hiyo anatoa maelezo ya kitendo hicho huku makada wakimvisha mavazi ya Chama Cha Mapinduzi.
Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM kutoka Lindi Mjini, Mama Salma Kikwete akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Mnazi Mmoja kilichoko
katika Kata ya Mingoyo walifurika kushuhudia sherehe za mbio za
pikipiki za uzalendo kusherehekea miaka 50 ya Mungano .
Wasanii wa Kata
ya Mingoyo wakitoa burudani wakati wa sherehe ya mbio za pikipiki
kusherehekea miaka 50 ya Mungano zitakazofikia kilele Aprili 26.
Mjumbe
wa NEC wa Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiwasalimia wananchi wa
Kijiji cha Madangwa na wageni waliohudhuria sherehe ya kupokea mbio za
pikipiki kwa Mikoa ya Kanda ya Kusini inayojumuisha Ruvuma, Mtwara na
Lindi katika kusherehekea miaka 50 ya Mungano.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama
Salma Kikwete akimjulia hali mtoto Seleman Salum Namputa, miezi 3,
aliyelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Lindi, Sokoine. Kulia ni Mama
mzazi wa mtoto Seleman ajulikanaye kama Mariam kutoka katika kijiji cha
Moka huko Lindi Vijijini. Mama Salma alitembelea hopitalini hapo.
Mama Salma, akizungumza wakati wa mkutano huo. PICHA NA JOHN LUKUWI.
0 comments:
Post a Comment