Home » » Karibu Mkoa wa LINDI: VIFAHAMU VIVUTIO VYA UTALII MKOA WA LINDI

Karibu Mkoa wa LINDI: VIFAHAMU VIVUTIO VYA UTALII MKOA WA LINDI


Mkoa wa Lindi ni miongoni mwa Mikoa michache yenye uoto wa asili

Mkoa wa Lindi ni miongoni mwa Mikoa michache ambayo uoto wake wa asili haujaharibiwa. Jitihada zinaendelea kufanyika kulinda uoto huu usiweze kuharibiwa kutokana na shughuli za wanadamu. Eneo la misitu iliyohifadhiwa ni kilometa za mraba 7,128. kati ya eneo hilo kilometa za mraba 6,958 ni hifadhi za Taifa na 170 ni hifadhi za Halmashauri. Eneo lililohifadhiwa ni asilimia 11 ya eneo la Mkoa.
VIVUTIO VYA UTALII MKOA WA LINDI 
Mkoa wa Lindi una vivutio vingi vya utalii ukanzia mambo ya kale na ya kihistoria ya Kilwa kisiwani, Kilwa, Songosongo, Kilwa kivinje. Hifadhi ya Taifa ya Selouss, Hifadhi ndogo ya mto Nyange, Fukwe za bahari, ya Hindi, mapango ya Nang’oma, mabaki ya mnyama Dinosaurus yaliyoko Tendenguru na Liwale German Boma, makaburi ya mikukuyumbu – Liwale. Hifadhi ya selous ni kubwa duniani na maarufu kwani inawanyama wengi wa aina nyingi ambao sehemu nyingine wametoweka kama mbwa mwitu, tembo, mamba jamii ya ndege.
Hifadhi hii imewekwa na UNESCO katika orodha ya urithi wa Dunia – kwa uamaarufu wake zadi Utalii unaoendelea huko ni wa kuwinda katika vitalu vyake na picha kivutio hiki kwa sasa hakiingiliki kupitia Mkoa wa Lindi kwa kukosa miundo mbinu kama barabara, hoteli za kitalii Kilwa, Liwale na Lindi.
Vitalu vya kuwindia – Kilwa Kaskazini na kusini
Kuna maeneo ya mapori huria yaliyotengwa kilwa ya kuwindia wanyamaori yanayojulikana kama ‘hunting block’s. Hivi sasa mapori hayo watalii huwinda wakati wa msimu kutokea Dar Es Salaam.
Bwawa la Mto Nyange
Bwawa ili lipo katika pori la wazi la hifadhi ndogo ya Mto Nyange. Pori hilo lenye ukubwa wa 50 km2 lilipendekezwa kuwa Hifadhi ya Taifa mwaka 1975 kwa kukosa pesa halijaendelezwa.
Umaarufu wa pori hili ni kule kuwa na viboko wapatao 450 katika bwawa hilo, ambao wanokana kwa pamoja wakati wa mchana usiku hutoka hutawanyika kutafuta chakula nchi kavu wanyama wengine wanaopatikana ni pamoja na nyati, tembo,mamba, ndege maji, kima tumbili nk.
Mambo ya kale - Tendenguru
Katika tarafa ya mipango wilaya Lindi vijijini yanapatikana mabaki ya mnyama Dinosaurus. Mnyama huyo aliyekuwa na uzito tani 190 na urefu wa 27.6m. aliishi katika eneo hili miaka 65-208 millioni iliyopita.
Baadhi ya mabaki (fossils) ya mnyama hyo yalichukuliwa na kupelekwa kuhifadhiwa katika jumba la makumbusho la Berlin kabla ya uhuru wa Tanganyika. Sehemu nyingine duniani yanakopatikana mabaki ya mnyama huyo ni Mexico, Merikani, Andes, Argetina na Uingereza.
Liwale German Boma
Huko Liwale kuna Boma lilijengwa na Wajerumani. Boma hilo lipo bado limesimama wa ndani yake kuna gogo kubwa lilitumika kama “gate’’ na sasa limegeuka jiwe. Pia kuna vivuli vya watu 7 waliouwawa na Wajerumani waliopinga utawala wao.
Boma hili linaweza kufikika kwa urahisi kamabara bara toka kilwa itatengenezwa na ujenzi wa hotel za Kitalii – Liwale.
Mikukuyumbu Makaburi ya Wamisionari Liwale
Karibu 64 km toka Liwale kuelekea Kaskazini ya mji wa Liwale kuna makaburi ya wamisionari (Askofu na Masista) waliouawa na wenyeji kwa kupinga Utawala wa Kijerumani Mwaka hadi mwaka Wajerumani huja kuzulu makaburi haya.
Milima na misitu ya Rondo.
Milima ya Rondo yenye miinuko mikali na mabonde (escarpments) iliyofunikwa na msitu wa asili wenye wadudu – vipepeo visingepatikana sehemu nyingine duniani vinavutia Watalii.
Hali ya hewa ya huko Rondo ni mzuri ya baridi ni kivutio kwa sehemu ya pwani yenye joto.
Misitu ya Mikoko
Pwani ya Lindi, Kilwa ina misitu ya miti ya mikoko ambayo ilitumika katika ujenzi wa nyumba Kilwa. Nyumba hizo zilizojengwa na mikoko karne ya 14 – 19 bado zingine zinztumika. Mikoko pia ilipelekwa Arabuni kujengea mshua na vyombo vingine vya bahari. Ukanda huu wenye mikoko takribani 26,500 umehifadhiwa na Serikali.
Kasa
Kasa hupatkana kwa wingi katika kanda ya Pwani ya Mkoa wa Lindi. Kasa hao huzaliana katika Fukwe za Songosongo, Shuka na Sudi. Aina zote saba za kasa wanapatikana katika Pwani hii Serikali ya Tanzania imewahifadhi kasa katika Sheria Na. 12 ya 1974 ya kuhifadhi Wanyama (W.C.A. 12/74)
Kisukuku – Coelacanth
Samaki huyu aliyeishi miaka 65 miliioni iliyopita alipatikana Kilwa na amevuliwa mara mbili samaki huyo aliyetoweka kumewafanya wanabaoogia kuamani kuwa samaki huyo Coelacanth ni nyumba ni kwake – pwani ya Kilwa inatazamiwa wanasayansi wengi kuja kufanya utafiti.
Spot za baharini
Maji ya wani ya ukanda wa Bahari ya Hindi ni mazuri kwa kupiga mbizi. 
Maji haya hayakuharibiwa, mtu anaweza kuona mpaka mita 30. Pia kuna “Sport Fishing” Samaki wanaovuliwa ni papa, samsuli, jodari, chewa na songoro.
Magofu ya Kilwa na Ustaarabu wa Pwani
Kilwa Kivinje, Kilwa Kisiwani na Songo Mnara kuna vivutio vikubwa kwa watalii wakitembelea huko. Katika mji wa kilwa na Kilwa Kisiwani kuna magofu ya Utawala wa Sultani wa karine ya 14 hadi 19.
Kilwa Kisiwani kuna magofu ya msikiti wa karine hizo ambao ulikuwa mkubwa na maarufu kuliko yote katika Afrika ya Mshariki. Utawala wa Sultani pia ulikuwa na hela zake. Biashara kubwa iliyokuwa inaendeshwa na waarabu hao iikuwa dhahabu meno ya tembo na utumwa. Habarihizi za kibiashara ziliwavuta wareno ndipo akatumwa Vasco Da Gama kuja kupeleleza.
Kwa kutembelea Kilwa Kisiwani Mtalii pia tajionea ngome ya Wareno iliyojengwa katika karne ya 14.
VIKWAZO VYA UTALII LINDI.
Ili utalii uweze kuendeshwa katika mkoa huu kunahitajika mambo kadhaa kama:-
Miundo mbinu ya mawasiliano, mahoteli ya kisasa, usafiri wa anga wan chi kavu na bahari na wakazi wake kuwa tayari kuwapokea watalii na kufanya kazi vizuri katika maeneo ya huduma za kitalii. Baadhi ya huduma hizo Serikali kuu imetoa kwa mfano ujenzi wa daraja la Mkapa na ujenzi wa barabara ya Mingoyo Lindi Kibiti ambao unaendelea.
Mahoteli na nyumba za kulala wageni
Miji ya mkoa huu haina hoteli za kutosha na za kisasa vivutio vya Utalii. Lindi mjini hakuna Hoteli ya Kitali. Zilizopo hazipo katika “Standard” ya juu. Hazina uchaguzi wa chakula maji yake ya kuchota nay a shida umeme nao sio wakuaminika. Hali hii pia imeikumba wilaya ya Liwale. Kilwa kuna hoteli chache zinazotoa huduma kwa Watalii.
Usafiri
Hakuna usafiri wa kuamnika toka Dar es Salaam hadi Kilwa, Lindi na Liwale. Safari tours zinahitajika. Panatakiwa pia usafiri wa boti toka Kilwa masoko kwenda Kilwa Kisiwani halikadhalika wa kwenda songo Mnara.
Usafiri wa anga na viwanja vya ndege
Kiwanja cha ndege cha Kikwetu cha Lindi mjini ni kizuri na kinatumika hata kwa ndege kubwa. Kinachotakiwa ni huduma ya usafiri toka uwanjani kuja mjini Lindi.
Uwanja wa Kilwa ni mdogo tena upo katikati ya mji. Uwanja mya unatakiwa uengwe nje kidogo ya mji (Maoni ya mwandishi).
Vivutio vya mafuta.
Kunahitajika vituo vingi vya mafuta mjini Lindi, Nangurukuru, Kilwa na Liwale. Pia ni busara kuwa na kituo cha mafuta kati ya Nangurukuru na Liwale, ingefaa Njinjo kungejengwa kituo hicho. Vituo vichache vya mafuta vilivyopo vinaendeshwa na matajiri wenye mitaji midogo na mara kwa mara huishiwa mafuta. 


0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa