Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
ELIMU bora haiwezi kupatikana mkoani Lindi kama hakutakuwapo mikakati
maalumu kuondoa tatizo la shule zilizojengwa kwa udongo, miti na
ukosefu wa vyoo katika shule za msingi zenye zaidi ya miaka 30,
imeelezwa.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Jordan Rugimbana ameyasema hayo jana wakati
alipozungumza na vyombo vya habari ofisini kwake na kueleza kuwa kuna
shule za msingi zina matatizo mbalimbali ikiwemo wanafunzi wanasoma
chini miti, vyumba vyao vya madarasa bado vya udongo na ukosefu wa vyoo.
Uongozi wa mkoa sasa unatakiwa kuhakikisha tatizo hilo linawekewa
mikakati ili kuondoa tatizo hilo la muda mrefu nalo ni moja ya chanzo
cha kushuka kwa elimu kutokana mazingira yake siyo mazuri ya kusomea.
“Mamlaka zote zinatakiwa kuhakikisha zinafanya kazi zake kwa
ushirikiano wa kutosha kuweza kuondoa kero hizo kila moja kuanzia ngazi
ya Mkoa, Halmashauri za Wilaya na Manispaa.
Haiwezekani wanafunzi wasome chini ya miti, udongo au nyumba ya
mwalimu ya udongo halafu useme kuwa inatakiwa kuwapo elimu bora kwa
wanafunzi itakuwa ni ndoto,” alisema.
Aidha, aliongeza kuwa tatizo hilo linaendana na la afya kwa vifo vya
mama na mtoto, navyo vinaleta athari mbaya kwa mkoa kutoka kituo cha
tiba kwenda kijijini ni hatua. Rugimbana alisema vifo hivyo vinatokea
njiani kwani mama akishafikia wakati wa kujifungua au mtoto anahitajika
kwenda hospitalini au kituo cha afya, hapo kuna umbali kwa bahati mbaya
anafariki.
Alisema ni wajibu wa mamlaka husika kuona tatizo hilo na kuchukua
hatua za kuliondoa kutokana na kupunguza nguvu kazi kwani unapompoteza
mama au mtoto unapoteza moja ya fursa za uchumi.
CHANZO : HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment