Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KAYA 200 kutoka kitongoji cha Namadingula katika Kata ya Rasibura
mjini Lindi wilayani humo wameharibiwa makazi, mashamba ya mazao ya
mahindi na ufuta kutokana mvua zinazoendelea kunyesha mjini hapa.
Diwani wa Kata ya Rasbura, Abdallah Kikwei aliyasema hayo jana wakati
akizungumza na gazeti hili ofisini kwake mjini hapa, na kueleza kuwa
wakazi hao walikumbwa na kadhia hiyo baada ya kunyesha mvua kubwa
iliyoambatana na upepo mkali usiku wa juzi kuamkia jana.
Hali hiyo inaendana na ya ukosefu wa vyakula, hivyo itasababisha
kuwapo njaa kwa wakazi hao kutokana vyakula vyao ambavyo vilihifadhiwa
ndani kwa ajili ya matumizi yao kila siku vilichukuliwa na maji.
Alifafanua uongozi wa kata uliamua kwenda kufanya ukaguzi na kubaini
tatizo hilo, na watapeleka taarifa kwa uongozi wa wilaya kuwasaidia
wakazi hao kwa makazi na mahitaji mengine.
Hata hivyo, alisema mpaka sasa yeye atapeleka tani 200 za mahindi kwa
ajili ya kuwapatia mbegu na tani 100 kwa zao la ufuta ili msimu
unaokuja kuendelea kulima mazao hayo. Kikwei alisema mvua hiyo iliathiri
wakazi wa Mitwero Stendi kutokana na baadhi ya nyumba kujengwa karibu
na njia ya maji yanayotoka katika mto na nyumba zao ziliharibika.
Aliongeza kuwa nyumba kadhaa za maeneo hayo ziliingiliwa na maji hayo
hususan ya mto Mitwero ambayo yanapofurika huwa yanapita kwenda baharini
CHANZO : HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment