Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
VYAMA sita vya msingi vya ushirika wilayani Liwale mkoani hapa
vinadaiwa na wakulima Sh mil 700 kutokana na kukusanya korosho bila
kuwalipa katika msimu wa 2015/2016.
Mwenyekiti wa kamati ya muda inayosimamia vyama vya msingi vya
ushirika katika wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale (RUNALI), Azizi
Liega, aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na gazeti hili
mjini hapa.
Alisema, madai hayo ni kwa ajili ya mauzo ya tani 350 kati ya tani
19,000 za korosho zilizokusanywa na vyama hivyo na kupelekwa katika
maghala kwa mauzo.
Mwenyekiti huyo wa kamati ya muda alifafanua kuwa, deni hilo kwa
vyama hivyo linatokana na kuuza korosho kwenye mnada mwezi uliopita na
kupatikana wanunuzi, lakini hawakuweza kutoa fedha kwa wakati
unaotakiwa.
Alisema, hali hiyo ilichelewesha malipo kwa wakulima hao na vyama
kubaki na deni, lakini bado korosho zipo katika maghala mpaka hapo
wanunuzi hao watakapofika na kulipa.
Alisema kampuni zilizoahidi kulipa zitafika Ijumaa wiki hii na kulipa
deni hilo ili kuzichukuwa korosho hizo tayari kuzisafirisha ndani na
nje ya nchi.
CHANZO : HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment