Chama cha Kuuza na Kununua Mazao cha Umoja, kilichopo wilayani
Liwale, Mkoa wa Lindi kimeanza kutekeleza mradi wa kugawa mbegu za
alizeti na ufuta kwa wakulima zaidi ya 700 zenye thamani ya Sh6 milioni.
Mwenyekiti wa chama hicho, Hassan Mpako alisema hayo jana katika uzinduzi wa mpango huo.
Alisema lengo lao ni kuwawezesha wakulima kulitumia zao hilo mbadala wa korosho na ufata.
Mpako alisema wakulima watafaidika kutokana na
kuwezeshwa kiteknolojia, ikiwamo kupewa mashine na utaalamu wa
utayarishaji wa mafuta ya alizeti.
Alisema kwa awamu ya kwanza, mradi huo utatekelezwa katika kata za majaribio za Nangando, Liwale na Likongowele.
Alisema hali hiyo itasaidia kubaini na kupunguza
vikwazo wanavyopata wakulima wa korosho ili waone namna ya kutumia fursa
nyingine badala ya kuendelea kuilaumu Serikali kwa kukosa soko la
korosho.
Katibu Tawala Wilaya Liwale, Jocob Nyamanga
aliwataka wakulima hao kutumia fursa hiyo kuongeza uzalishaji ili
kujipatia mapato ya ziada.
“Mpango huu ni mzuri, hivyo ni vyema vyama vyote
vya ushirika vikaiga utaratibu Chama cha Umoja wa kuwapatia mbegu za
alizeti wanachama wao,” alisema Nyamanga.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment