Wakazi
wa kijiji cha kitwavi kilichopo katika kata ya matimba halmashauri ya
lindi vijijini wameilalamikia serikali kufuatia kuapishwa mgombea wa
nafasi ya uenyekiti wa kijiji hicho kwa tiketi ya CCM kuwa mshindi
katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa madai kuwa mshindi halali
alikuwa mgombea kutoka chama cha wananchi CUF.
Wakizungumza na ITV wakazi wa kijiji hicho wamesema hawatomtambua
wala kumpa ushirikiano mgombea wa chama cha mapinduzi endapo ataapishwa
kuwa mwenyekiti, kwa kuwa awali msimamizi wa uchaguzi katika kijiji
hicho alishamtangaza mgombea wa CUF kuwa mwenyekiti wa kijiji hicho
ambapo pia wanakijiji hao wameleeza kushangazwa na kitendo cha mgombea
wa CCM kuhudhuria shughuli ya kuapishwa ikiwa mshindi alikuwa mgombea wa
CUF na kwamba maelelezo ya msimamizi wa uchaguzi kijijini hapo hayana
ukweli wowote.
Msimamamizi wa uchaguzi katika kijiji hicho ambaye amekiri
kumtangaza mgombea wa chama cha wananchi CUF kuwa mshindi na kuongeza
kuwa alilazimika kufanya hivyo kufuatia shinikizo lililotolewa na baadhi
ya wanachama wa chama cha wananchi CUF waliokuwa wamezingira wakiwa na
silaha za jadi jengo ambamo zoezi la uhesabuji kura za vitongoji vyote
vya kijiji hicho likiwa linaendelea ambapo pia amekanusha madai ya
kuwa mgombea wa CUF ndiye aliyeibuka mshindi na kwamba mgombea wa chama
cha mapinduzi ccm ndiye mshindi katika uchaguzi huo.
ITV ikamtafuta mkurugenzi wa halmashauri ya lindi vijijiini na
kuzungumza nae ambapo amesema kuwa, alipokea taarifa hizo na kwamba
taarifa ya kuwepo vurugu zilizopelekea kupotoshwa kwa taarifa za matokeo
katika kijiiji hicho licha ya kuwepo kwa ulinzi wa mgambo zipo katika
ngazi ya polisi wilaya, ambapo ameongeza kuwa hajapokea barua yoyote ya
kuitwa mahakamani licha ya walalamikaji kupewa muda wa kuwasilisha
malalamiko yao katika vyombo vya sheria.
Kwa matokeo ya awali yaliyotangazwa na masimamizi wa uchaguzi
kijijini hapo yalionyesha kuwa chama cha wananchi CUF katika nafasi ya
mwenyekiti ndicho kilichoibuka mshindi kwa kura 102 dhidi ya mgombea wa
CCM aliyepata kura 99, jambo linaloibua hali ya sintofahamu endapo
mgombea wa ccm ataapishwa kuwa mwenyekiti wa kijiji hicho.
Chanzo:ITV Tanzania
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment