Home » » MBUNGE WA CCM ATIMULIWA KIJIJINI AKIVIZIA JIMBO LA KADA MWENZAKE

MBUNGE WA CCM ATIMULIWA KIJIJINI AKIVIZIA JIMBO LA KADA MWENZAKE

Mbunge wa viti maalum (CCM), Zainabu Kawawa.
 
Baadhi ya wanakijiji cha Makinda wilayani Liwale mkoani Lindi, wamemtimua mbunge wa viti maalum (CCM), Zainabu Kawawa, baada ya kudaiwa kutaka kuitisha mkutano wa kutangaza nia ya kuomba ubunge katika jimbo hilo kabla ya wakati. Mbunge wa Liwale ni Faith Mtambo (CCM).
Tukio hilo lilitokea Alhamisi wiki hii, saa nane mchana baada ya mbunge huyo kufika kijijini hapo kwa lengo la kukutana na mwenyekiti wa kijiji, Salum Kachwele ili aitishe mkutano wa kujinadi.

Kachwele alitakiwa kuwakutanisha wajumbe wa serikali ya kijiji na baadhi ya wananchi hasa wazee maarufu, ili kuwashawishi wamuunge mkono katika harakati zake za kuwania ubunge wa jimbo hili.

Akizungumzia tukio hilo, mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Kachwele, alisema mbunge huyo alifika kijijini hapo akiwa na mpambe wake, Mkopora Mkopara na kumuomba awaite wajumbe wa serikali  ya kijiji  pamoja na wazee maarufu ili azungumze nao.

Hata hivyo, kikao hicho hakikufanyika kwani kabla ya kuanza harakati hizo, ilidaiwa kuwa mbunge Kawawa hajawahi kufanya kikao chochote wala kutembelea kijiji hicho.

Kachwela alisema  kabla ya mkakati wa kukutana na wananchi hao haujafanikiwa, lilikuja  kundi  kubwa likiongozwa na vijana waliokuwa na mawe, magongo mikononi, wakizomea na kupiga kelele.

Walikuwa wakitokea kwenye  mkutano wa Chama cha Wananchi (CUF), uliokuwa ukiwashukuru wananchi kwa kukichangua chama hicho kwenye uchagunzi wa serikali za mitaa na kumtaka mbunge huyo kuondoka katika eneo mara moja.

Kwa upande wake, mbunge Zainabu alikiri kutembelea kijiji hapo ila alikataa kutaka kikao na wananchi hao na kukanusha habari za tukio la kufukuzwa.
Alieleza kuwa alikwenda kufanya ziara ya kikazi ya kuwatembelea wapiga kura kuhamasisha maendeleo.

“Ndugu yangu hayo maneno si kweli, mimi nilikwenda kijijini hapo kufanya kazi za kibunge si kampeni kama ilivyoelezwa na hao watu wasionitakia mema, ukweli ni kwamba mti wenye matunda matamu ndiyo unaopigwa mawe”,  alisema Kawawa.
CHANZO: NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa