Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa 
Lindi Ndugu Regina Chonjo mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege 
wa Lindi tarehe 11.12.2014.
NGAPI???"Mbiliii;-Hivi ndivyo mke wa rais Mama Salma Kikwete, 
alipowauliza wana Ndaro kuhusu muundo gani wa serikali unaokubalika 
nchini, na kujibiwa serikali mbili.Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM na Mke wa 
Rais Mama Salma Kikwete akishirikiana na viongozi wa CCM wa Kata ya 
Ndaro kuunga mkono muundo wa serikali mbili unaopendekezwa na Rasimu ya 
Katiba, wakati akiwa kwenye kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa 
huko Lindi leo Alhamisi Desemba 11, 2014. Uchaguzi wa serikali za mitaa 
utafanyika kote nchini Desemba 14, 2014
Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete 
akishirikiana na viongozi wa CCM wa Kata ya Ndaro kuunga mkono muundo wa
 serikali mbili unaopendekezwa na Rasimu ya Katiba, wakati akiwa kwenye 
kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa huko Lindi leo Alhamisi Desemba
 11, 2014. Uchaguzi wa serikali za mitaa utafanyika kote nchini Desemba 
14, 2014
Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi wa 
Wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akisalimiana na viongozi wa CCM
 Kata ya Mikumbi iliyoko Mjini Lindi wakati alipowasili kwenye eneo hilo
 kwa ajili ya kufanya mkutano wa ndani na viongozi hao tarehe 
11.12.2014. Anayemtambulisha kwa wajumbe hao ni Mwenyekiti wa CCM wa 
Kata ya Mikumbi Bwana Bakari Seif Mikojo.
Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM anayewakilisha Wilaya ya Lindi Mjini na 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwatambulisha na kuwaombea kura 
wagombea uenyekiti wa serikali za mitaa wa Kata ya Ndaro kwa wajumbe wa 
mkutano. Mama Salma yuko Wilayani Lindi Mjini kuhamasisha wananchi 
kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa 
unaotarajiwa kufanyika tarehe 14.12.2014.
Picha na John Lukuwi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment