Home » » KIFARU CHAGONGA NYUMBA, CHAUA WATATU

KIFARU CHAGONGA NYUMBA, CHAUA WATATU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
KIFARU cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), jana kiliacha njia na kugonga nyumba mbili za
raia na kusababisha vifo vya watu watatu katika Kijiji cha Mnolela barabara kuu ya Mtwara Dar es Salaam.
Kifaru hicho chenye namba za usajili 018 mali ya JWTZ kikosi Namba 83, iliyokuwa inaendeshwa na askari wa jeshi hilo, Shadhil Nandonde, ikitokea Mtwara kwenda Nachingwea.
Ajali hiyo ilitokea majira saa 11:30 alfajiri na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo askari Namba Mt 10728 Private Pascal Komba na Somoe Kamteule (75), mkazi wa Mnolela ambaye alikuwepo ndani ya nyumba moja kati ya zilizogongwa.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, Renatha Mzinga, majeruhi wa ajali hiyo ni MT. 10744 Private Simon Edward, MT. 106842, Private Feruz Haji, MT. 1077263 Private Omary Makao, MT. 99018 Private Mbaruk Duch, MT. 107442  Private Simon Masele na MT. 107218 Private Ndekenya.
Kifaru chagonga nyumba, chaua watatuMajeruhi walikimbizwa hospitali ya Rufaa ya Ligula kwa ajili ya matibabu zaidi.
Kwa upande wake, Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Dk. Lobikieli Kisambu, alithibitisha kwa njia ya simu kuwa alipokea maiti mbili na pamoja na mejeruhi sita.
Kwa mujibu wa Dk. Kisambu, kati ya majeruhi hao waliyopokelewa hospitalini hapo, mmoja amepelekwa hospitali ya Nyangao kutokana na hali yake kuwa si ya kuliridhisha na mmoja wao amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu na kufanya waliofariki kufikia watatu.
 Chanzo; Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa