Home » » Watu watatu wamefariki Dunia baada ya Magari mawili yenye tela kila moja kuacha njia na kupinduka

Watu watatu wamefariki Dunia baada ya Magari mawili yenye tela kila moja kuacha njia na kupinduka

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Watu watatu wamefariki Dunia baada ya Magari mawili yenye tela kila moja kuacha njia na kupinduka na kufasabisha vifo vya watu hao na kujeruhi wengine wawili katika ajali iliyotokea Jana Huko Tarafa ya Rondo wilaya ya Lindi Mkoani Lindi.

Ajali hiyo Iliyohusisha gari aina ya HOWO lenye Usajili T270BZU na Tela na T260AZU Pamoja na Lori aina HOWO T871 BTH Tela T 626 BTT yote yaliacha njia

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi kamishna msaidizi Renatha Mzinga amethibitsha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja marehemu hao ambao ni Marehemu Jackson Francis Kayombo (DEREVA) mwenye umri wa miaka 42,marehemu Lazaro Michael Chaula,(Mkinga) miaka 27 Dereva na Marehemu Mohamed Jumanne Said (Mmakonde) miaka 23.

Kamanda Mzinga amewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni ambao ni Given Mussa Mohamed na Seleman Ibrahim Hamis ambapo pia alibainisha kuwa Maiti na majeruhi wote wamefikishwa katika Hospital ya Sokoine Manispaa ya Lindi.

Aidha kamanda Mzinga pia alieleza matukio ya mwishoni mwa wiki ambapo Wakazi wanne wa wilaya za Nachingwea,Ruangwa na Manispaa ya Lindi, wamefariki dunia katika matukio tafauti,likiwemo mtu anayesadikiwa kuwa na matatizo ya akili kuwapiga vikongwe wawili mwishoni mwa wiki iliyopita mkoani hapa.

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa