Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
MFUKO wa Taifa wa  Bima ya Afya (NHIF) mkoani Tabora, umeikabidhi 
Hospitali ya Rufaa Kitete msaada  wa shuka 150 zenye thamani ya sh 
milioni 3.5.
  Akikabidhi msaada  huo, Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Balozi Ali Mchumo, alisema kuwa wataendelea  kutoa msaada kulingana na
mahitaji ili kukabiliana na changamoto katika Hospitali ya Rufaa Kitete.
mahitaji ili kukabiliana na changamoto katika Hospitali ya Rufaa Kitete.
  Mchumo alisema  mfuko utaendelea kufanya hivyo kwani wao wana wajibu 
wa kutoa misaada kwa ajili  ya kuwawezesha wagonjwa kupata huduma nzuri.
  Alisema kuwa shuka  hizo zitapunguza adha ya wagonjwa kutumia kanga na vitenge kwa ajili ya  kujifunika.
  Akikabidhi msaada  huo kwa Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. 
Dennis Kitapondya, Mchumo  alisema kama mfuko wamejipanga kuendelea 
kusaidiana na hospitali na vituo vya afya  ili kukabiliana na changamoto
 zinazowakabili.
  Kuhusu uchakavu wa  majengo na upungufu wa miundombinu, Mchumo 
aliutaka uongozi wa hospitali hiyo  kukopa kutoka katika mfuko huo kwani
 hivi sasa wanakopesha vifaa mbalimbali,  vikiwemo vipimo na vile vya 
ukarabati ili kuweza kutoa huduma nzuri.
  Awali Dk.  Kitapondya akitoa taarifa fupi kwa mwenyekiti wa Bodi ya 
NHIF, alisema  wanakabiliwa na upungufu wa miundombinu ambayo imekuwa 
ikisababisha msongamano  na kusababisha wagonjwa kulala wawili katika 
kitanda kimoja.
  Pia aliongeza kuwa  wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa watumishi, hasa
 madaktari, na kwamba uongozi  wa mkoa kwa jitihada zake uliweza 
kuipatia hospitali hiyo madaktari 12 mwaka  jana ambao hata hivyo 
alisema hawatoshelezi.
  Katibu Tawala wa  Mkoa wa Tabora, Kudra Mwinyimvua, aliishukuru NHIF 
kwa msaada huo akisema kuwa  hospitali hiyo ina vitanda 350 na shuka 
zilizokuwepo ni 150 tu.
Chanzo:Tanzania Daima 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment