Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAZAZI na walezi wa wachezaji wa timu ya Lindi Soccer Academy
(LSA), ya mjini hapa, wamebariki ushiriki wa kikosi hicho katika
michuano ya mwaka huu ya vijana ya Rollingstone kwa nchi za Afrika
Mashariki na Kati chini ya mwamvuli wa East and Central African Youth
Football Academies Association (ECAYFA).
LSA imealikwa kushiriki michuano hiyo ya vijana chini ya miaka 20 na
15 itakayofanyika kuanzia Julai 5- 14 kwenye viwanja vya Karume Ilala
na Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.
Wazazi hao walikubaliana kwa kauli moja katika mkutano uliofanyika
ukumbi wa Double M Hotel, kuiwezesha LSA kushiriki michuano hiyo,
ambapo waliafiki kuchangia gharama mbalimbali ikiwamo nauli, malazi na
chakula, huduma ambazo timu za Tanzania zinapaswa kujigharamia zenyewe
wakati wa mashindano.
Watu 50 wakiwamo wachezaji, viongozi na wazazi, walishiriki mkutano
wa kujadili masuala mbalimbali yanayoihusu LSA, ukiwamo mradi wa ujenzi
wa shule, viwanja na kituo cha michezo cha timu hiyo, utakaofanyika
Kilangala, Lindi Vijijini, ambako wamepata eneo la ujenzi.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment