Home » » Sido yatoa mikopo kwa wajasiliamali wa mkoa wa Lindi

Sido yatoa mikopo kwa wajasiliamali wa mkoa wa Lindi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Meneja wa Sido mkoa wa Lindi,Mwita Kasisi akieleza
jinsi shirika lake linavyowezesha wajasilamali wa mkoa huo kwa kuwapa
mikopo na elimu ya wajasiliamali katika hafla Fupi ya kukabidhi hundi
za mikopo kwa wajasiliamali 21,kutoka kushoto ni Bw Dickson
Kindole,Mhandisi Sido,Bi Salma Ally,Afisa mikopo na Mkuu wa Wilaya ya
Lindi Dr Nassor Hamid
 Baadhi ya wajasiliamali waliokabidhiwa hundi za mikopo
wakimsikiliza Mkuu wa wilaya( hayupo pichani)Katika Hafla hiyo
iliyofanyika jana mjini Lindi
 Mkuu wa Wilaya ya Lindi,Dr Nassor Hamid akikabidhi Hundi kwa
Bi Fatuma Hamis katika hafla ya kukabidhi hundi kwa wajasiliamali wa
mkoa wa Lindi
 Bw Abdallah Mbinga akipokea Hundi ya mkopo toka kwa mkuu wa
wilaya ya Lindi,Dr Nassor Ally Hamid

 Picha ya Pamoja kati ya Mkuu wa Wilaya ya Lindi na Watumishi
wa sido wakiwa na wajasiliamali waliowezeshwa na shirika hilo kwa
kupatiwa mikopo ya kujiendeleza kibiashara
========   ========  =======
Na Abdulaziz ,Lindi
Jumla ya Tshs Milioni 42.5 zimetolewa kwa Wajasiliamali  21 wa Mkoa wa
Lindi katika Kuimarisha Biashara  ikiwa ni nyongeza ya Mikopo
inayotolewa na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo(SIDO)Chini ya Mpango
unaowezeshwa  katika kusaidia Jamii kujitegemea ikiwemo kuchangia
maendeleo.

Akisoma taarifa ya Shirika hilo wakati wa kukabidhiwa Hundi kwa
Wajasiliamali hao  Meneja wa Mkoa,Mwita Kasisi  ameeleza kuwa mkopo
huo ni mfululizo wa mikopo iliyoyotolewa kwa wajasiliamali 1328
kuanzia  mwaka 1994.

Kasisi alibainisha kuwa  lengo kuu la kutoa mikopo ni kukuza na
kuendeleza viwanda vidogovidogo pamoja na kuboresha masoko ya Bidhaa
zinazozalishwa na wajasiliamali wadogo kwa kupandisha thamani ya mazao
ikiwemo zao la Ufuta na korosho.

Aidha Kasisi alisema kwa sasa Shirika linaendelea kujikita katika
kuhakikisha wajasiliamali wanapata ushauri na mafunzo ya aina
mbalimbali, ili kujiweka tayari kwenye ukuzaji wa viwanda vidogovidogo
.
Akiongea na wajasiliamali hao kabla ya kukabidhi Hundi kwa
wajasiliamali hao 21,Mkuu wa Wilaya ya Lindi,Dr.Nassoro Ally Hamidi
amewataka wajasiliamali hao kuitumia mikopo hiyo kwa malengo
yaliyokusudiwa ili  kuendeleza na kukuza mitaji yao kufuatana na
mifumo ya Ubora ili kupata soko zuri la Bidhaa zao
Aidha Dr Hamid alisema kuwa Mikoa ya Lindi na Mtwara kwa sasa
inaimarika kibiashara kutokana na ugunduzi wa Nishati ya Gesi hivyo ni
lazima wafanyabiashara wajipange kuimarisha ubora wa bidhaa zao ili
kupata soko na kuondoa ulazima wa kuagiza bidhaa toka katika mikoa
mingine na nje ya Nchi
Kwa upande wao baadhi ya wajasiliamali wameiomba Serikali kuendeleza
elimu ya Kibiashara kwa wajasiliamali ikiwemo kuwawezesha kwa mikopo
yenye riba nafuu ili kumkomboa mlaji mwenye kipato kidogo huku
wakiitaka Mamlaka ya Mapato kuangalia viwango vya kodi kulingana na
ukubwa wa biashara za wajasiliamali wadogo
Hafla hiyo ya kukabidhi hundi hizo imefanyika katika ofisi za shirika
hilo mkoani Lindi

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa