Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetangaza hatari ya
kuwapo kwa mvua kubwa zitakazoambatana na upepo kuanzia Februari 11 hadi
13.
Taarifa iliyotolewa na TMA, inasema kiwango cha mvua hizo kinatarajiwa kuwa zaidi ya milimita 50 kwa saa 24 mfululizo.
Inaendelea kuwa mabadiliko hayo ya hali ya hewa
yanasababishwa na kimbunga kilichotokea kandokando ya pwani ya Bahari ya
Hindi, kilichotokea Pwani ya Somalia na Misitu ya Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Watu wa Kongo.
Miongoni mwa mikoa iliyo katika hatari ya kukumbwa
na hali hiyo, ni Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Lindi, Mtwara, Morogoro,
Mbeya, Ruvuma na Visiwa vya Unguja na Pemba.
Kutokana na hali hiyo, wakazi wa maeneo hayo na
watumiaji wa bahari wametakiwa kuwa waangalifu kuepuka madhara yoyote
yanayoweza kujitokeza.
Katika mvua iliyonyesha juzi, inaripotiwa kusababisha madhara Mikoa ya Dar es Salaam na Kilimanjaro.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment