Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimezidi kujizolea viti vya udiwani kata mbalimbali ikiwamo Ludewa, Tarafa ya Kimamba, wilayani Kilosa, mkoani Morogoro na Mkongoro, Wilaya ya Kigoma, mkoani Kigoma.
Juzi, CCM kilikuwa kimeshakutwaa Kata 23 huku Chadema kikinyakua vitatu wakati NCCR-Mageuzi iliambulia moja.
Kata ya Ludewa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya Kilosa, Masalu Mayaya alimtangaza mgombea wa CCM, Subiri
Mwamalila kuwa mshindi kwa kuwashinda wagombea wenzake kupitia Chadema
na Cuf.
Naye Msimamizi wa Uchaguzi Kata ya Mkongoro,
Wilaya ya Kigoma,, Shija Lyela alimtangaza Morani Hussein wa CCM kuwa
mshindi kwa kujizolea kura 1,496 akiwashinda wapinzani wake saba
waliojitokeza kuwania udiwani kata hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Diwani
wa Chadema kuanzia mwaka 2010 ilipoanzishwa.
Kutokana na ushindi huo wa CCM katika kata 23
katika uchaguzi mdogo wa madiwani ulioshirikisha kata 27 nchini, wasomi
nchini wametoa sababu nne zilizosababisha chama hicho kuibuka na ushindi
kuwa ni; Utawala bora wa Sekretarieti Mpya ya CCM.
Pia, kutumia nafasi ya kujiimarisha ndani ya
mgogoro wa Chadema, vyama vya upinzani kutokuwa na wanachama vijijini na
kutofanyiwa maboresho kwa daftari la kudumu la wapigakura.
Wakati wasomi hao wakieleza hayo, Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema ushindi huo unatokana na
chama hicho kuwatumikia zaidi wananchi. Kauli hiyo ya Nape ilipingwa na
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ambaye
alidai kuwa chama hicho tawala kimetumia dola ndiyo maana kimefanikiwa
kushinda uchaguzi huo.
Lipumba anena
Kwa upande wake Profesa Lipumba alisema CCM
kimetumia dola ndiyo maana kimeshinda, huku akitolea mfano kata ya
Kiwalala mkoani Lindi na Kiomoni mkoani Tanga.
“Kiomoni watu wamezuiwa kupiga kura, na Kiwalala aliyeshinda alikuwa na kesi. Pia Nec imeisaidia CCM kupata ushindi” alisema.
Profesa Lipumba alisema tabia ya chama hicho
kutumia dola katika uchaguzi kinaweza kuibua vurugu nchini iwapo
wananchi watachoshwa na hali hiyo, “Ili ushinde uchaguzi nchini
inatakiwa uingie katika mapambano makubw ana vyombo vya dola
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi,
Leticia Ghati alisema kuwa chama hicho kimeshinda kutokana na kuwa na
ngome nzuri mkoani Kigoma, “Kata tuliyoshinda diwani alikuwa wa NCCR
hivyo tulijua tu kuwa tutaibuka na ushindi.”
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment