Home » » TUKIO KATIKA PICHA; NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO LINDI

TUKIO KATIKA PICHA; NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO LINDI


Nyumba ya moja mali ya Mzee Nampembe,Mkoani Lindi. imeteketea kwa moto jana Usiku na kupelekea baadhi ya mali zilizokuwemo ndani ya nyumba huyo kushindwa kuokolewa. Hali hiyo ilipekekea Wananchi wa eneo la jirani na nyumba hiyo kupiga mawe gari la zimamoto baada ya kuchelewa kufika eneo la Tukio kwa ajili ya kuzima moto huo.
Mmoja kati ya wakazi wa nyumba hiyo amepoteza fahamu toka jana baada ya kupatwa na Mshituko. Chanzo cha Moto imeelezwa kuwa ni Mshumaa baada ya kukosekana Umeme mjini Lindi usiku wa jana.
Picha na Abdulaziz Video, Lindi
Wasamalia waliokuwepo eneo la tukio wakisaidiana kumbeba mtu mmoja aliepoteza fahamu baada ya kutokea kwa tukio hilo.
Vilio vilitawala wakazi wa nyumba hiyo baada ya kutokea kwa tukio hilo.
Sehemu ya mali zilizookolewa.
PICHA KWA HISANI YA MICHUZI BLOG

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa