Lindi.Wafanyabiashara wa Manispaa ya Lindi,
wamegoma kutoa huduma kwa kufunga maduka kwa kile walichodai wamechoshwa
na kero mbalimbali wanazofanyiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Tukio hilo lilitokea juzi baada ya wafanyabiashara
hao kufanya kikao na kuamua kufunga maduka kwa siku saba, ili
kushinikiza TRA kuacha tabia ya kuwabugudhi.
Mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara hao, Hamis
Livembe alisema wameamua kufanya hivyo kutokana na kulazimishwa kutumia
mashine inayouzwa Sh800,000, huku walio wengi wana mitaji midogo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dk Nassoro Himid
alikiri kufahamu na kwamba, wanalifanyia kazi haraka ili hali hiyo
isijitokeze tena ndani. Pia, juzi baadhi ya wafanyabiashara soko kuu
waliamua kupanga bidhaa chini.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment