Home »
» Kilwa Kivinje yakua kwa kasi
Kilwa Kivinje yakua kwa kasi
JIBU LA SWALI LA MBUNGE Kilwa
|
|
|
SERIKALI imesema suala la kupandisha hadhi mji na kuwa
halmashauri ya mji mdogo linatokana na makubaliano kati ya Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na halmashauri husika.
Hayo yalielezwa bungeni jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia, alipokuwa
akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Suleiman Bungara
(CUF).
Ghasia alisema jambo hilo linategemea kwanza wapate maombi kutoka
katika halmashauri husika ambayo mpaka sasa hawajayapata, hivyo
kushindwa kujua kama wana vigezo ama la.
“Mara halmashauri husika itakapoleta maombi kwetu sisi tutajua kama
eneo husika lina vigezo vya kupandishwa hadhi na kuwa mji mdogo na
kukamilisha zoezi hilo kwa haraka,” alisema Ghasia.
Alikiri ipo kasi ya ukuaji wa idadi ya watu katika mji wa Kilwa
Kivinje ambayo inaleta changamoto katika utoaji wa huduma za jamii
katika eneo hilo.
Alisema kwa kuzingatia hilo, serikali ilitangaza mji huu kuwa eneo la
mipango kupitia Tangazo la Serikali Na. 176, la Agosti 9, mwaka 1996
ili kuzuia ukuaji holela, kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha
huduma za jamii.
Katika swali lake mbunge huyo alitaka kujua ni lini zoezi la
kukamilisha Kilwa Kivinje litakamilika, lililoulizwa kwa niaba yake na
Mbunge wa Ole, Rajabu Kasim Mbarouk.
CHANZO;TANZANIA DAIMA
|
|
0 comments:
Post a Comment