Ruangwa.Wanachama wa Chama cha Ushirika cha
Msingi Luchelegwa, Wilaya ya Ruangwa, Mkoa wa Lindi, wamelalamikia
uongozi wa halmashauri hiyo kwa kuwaondoa madarakani watendaji wao kwa
madai ya kutumia gari la Chuo Kikuu cha Ushirika cha Mkoa Ilulu,
kusambaza fedha za kununulia korosho.
Akizungumza kwa niaba ya wakulima na wanachama wa
chama hicho, Somoe Liuna alisema wakulima wa korosho hawatambui uongozi
uliowekwa na viongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo. (Mwanja Ibadi)
kwa maslai yao ya kisiasa.
Somoe alisema kitendo hicho cha halmashauri
kuingia uhuru wa vyama vya ushirika ni kuvunja sheria ya ushirika
kifungu 20 cha mwaka 2000 na kinawakatisha tamaa wakulima kujiunga
kwenye vyama hivyo.
Fabiani Nguli diwani wa kata ya Chinongwe alisema
kuwa mgogoro wa chama cha ushirika Luchelengwa umetengenezwa na
mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Ruangwa Issa Libaba kwa lengo la
kukidhahofisha chama hicho chenye mafanikio makubwa ya kiuchumi.
Nguli alisema mwenyekiti huyo anatumia nafsi yake
vibaya kwa maslai yake binafsi anasahau maslai ya umma maana mgogoro
alioutengeneza unalengo la kuwaumiza wakulima wasiona hatia wasiuze
mazao yao kwa wakati.
Alisema chama cha ushirika Luchelegwa kimepata
mafanikio makubwa chini ya uongozi uliondolewa na mwenyekiti huyo hali
ambayo wakulima na wanachama hawaweza kukubalina na maamuzi yake.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya
wilaya Ruangwa Issa Libaba alikiri kuwepo kwa mgogoro katika chama hicho
lakini alikanusha kuwa mgogoro huo haujasababishwa na viongozi na
watendaji wa halmashauri hiyo.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment