Migogoro,
mivutano na malumbano ya mara kwa mara ya watendaji wakuu wa kata na
vijiji na viongozi wa siasa imetajwa kuwa ni kati ya sababu zinazofanya
baadhi ya miradi ya maendeleo kwenye halmashauri ya wilaya ya
Nachingwea kutotekelezwa kwa wakati.
Akisoma taarifa
ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha mwezi aprili na juni
mwaka huu kwenye kikao cha Baraza la madiwani la halmashauri hiyo, kwa
niaba ya Mkurugenzi wa halmashairi ya wilaya ya Nchingwea, Afisa mipango,James
Mbakile amesema kuwa hali hiyo inafanya watendaji hao kukosa muda
wa kusimamia miradi hiyo na kwa kiasi kikubwa kuwakatisha
tamaa na kuwafanya wakose ari na kujituma katika uwajibikaji.
Mbakile
ametaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na baadhi ya wakandarasi kutokuwa
wakweli na waaminifu katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi hivyo
kuchelewesha kazi na baadhi ya kazi kuwa chini ya viwango.
Na katika
kukabiliana na changamoto hiyo halmashauri imeendelea kutangaza kazi kwenye
vyombo mbalimbali vya habari ili kuwapata wakandarasi wa nje ya wilaya ili
kuleta ushindani katika kutekeleza miradi mingi ya maendeleo iliyopo
kwenye halmashauri hiyo.
Pia
amesema sababu nyingine ni kuchelewa sana kwa ruzuku ya maendeleo toka Serikali
kuu ambako huathiri kwa kiwango kikubwa kuanza kwa utekelezaji wa shughuli za
maendeleo.
0 comments:
Post a Comment