Home » » Wananchi wa Nachingwea Wajipanga kususia kituo cha mabasi

Wananchi wa Nachingwea Wajipanga kususia kituo cha mabasi



Basi zikiwa stendi

Na Abdulaziz Video,Lindi
Huku kukiwa na zaidi ya sh milioni 700 zikiwa zimeanza kutumika katika ujenzi wa kituo kipya cha mabasi cha wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi ambapo zoezi la ujenzi wa kituo kipya cha mabasi wilayani humo kuanza kujengwa na kutumika katika maeneo ya uwanja wa ndege,Baadhi ya Abiria leo wametishia kugoma kutokana na Kuzuia tena uwepo wa kituo cha karibu na maeneo ya Mjini kutokana na Umbali uliopo na kituo hicho kipya.

Hali hiyo imetokea leo asubuhi baada ya baadhi ya Abiria kugomea kituo hicho kipya kutokana na Halmashauri ya Wilaya hiyo kushirikiana na Jeshi la Polisi kufuta kituo cha Tunduru na kuagiza wasafirishaji wote kutumia kituo cha Stesheni kuwa cha mwisho njiani kabla ya kufika kituo kikuu ambapo kuna umbali mrefu hali inayofanya Abiria wengi kunufaisha watoa huduma za bajaj na Bodaboda huku wengine wakitembea Umbali Mrefu kwa kukipita msituni.

Akiongea na Mtandao huu Mwandishi wa Gazeti la Raia Mwema wilayani humo,Ahmaid Mmow alieleza kuwa hali hiyo imeleta kero kubwa kwa Abiria wanaosafiri kati ya Nachingwea,Masasi,Newala,Lindi na Dar es salam huku wengine wakisafiri wakiwa na shida mbalimbali za kijamii.

Abiria wengi baada ya kuanza kwa stand mpya waliumia sana na umbali na msitu uliopo lakini Halmashauri ilipoanzisha kituo cha Tunduru ya Leo kidogo kilileta ahueni sasa sijui ni kwa nini wamekifuta hali inayofanya abiria wengi kulazimika kutembea umbali mrefu wa zaidi ya km 5 hadi stand Mpya na stesheni.

 Hii inaumiza sana hasa wenye wagonjwa,Kufuatia hali hiyo Baadhi ya Mawakala wa Mabasi ya Abiria na Abiria wamedhamiria kuitisha maandamano ya kuhamasisha kutotumia kituo kipya kinachoendelea kujengwa hadi kitakapokamilika kutokana na kukosekana kwa baadhi ya huduma muhimu za kijamii ikiwemo mabanda ya kupumzikia Abiria.

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa