Home » » Kesi ya wasomali waliokamatwa na silaha za kijeshi yapigwa kalenda

Kesi ya wasomali waliokamatwa na silaha za kijeshi yapigwa kalenda

MAHAKAMA ya hakimu mkazi mkoani Lindi, imeahirisha hukumu ya kesi ya watuhumiwa wakisomali wanaodaiwa kukutwa na silaha za kijeshi katika kisiwa cha Mkuza wilayani Kilwa,  mkoani Lindi.

Watuhumiwa hao watano walikamatwa mwezi wa April, mwaka jana  wakiwa na bunduki tatu aina ya smg, risasi 264, mabomu ya kutupa kwa mkono na ya masafa marefu na RPG moja.

Wakili wa Serikali Juma Maige ameyasema hayo leo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisni kwake, mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo na hakimu mfawidhi wa mahakama ya haikimu mkazi Dastan Ndunguru.

Amesema kuwa watuhumiwa hao walishtakiwa kwa makosa mawili ya kuingia nchi bila ya kibali ambayo tayari wamekwisha kutumikia kifungo cha mwaka mmoja na kusalia na kosa la tuhuma ya kukutwa na silaha za kijeshi.

Wakili Maige amesema kuwa hukumu iliyotakiwa kutolewa leo, ya tuhuma za upatikanaji wa silaha, kwa bahati mbaya mkalimani wa lugha ya kisomali hakufika kutokana kilichotajwa kuwa amesafiri.

Almetaja kuwa kesi hiyo yenye namba 42  ya mwaka  2012  ambapo hukumu itatolewa wikimbili zijazo baada ya kurudi mkalimani huyo, na watuhumiwa bado wako rumande.

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa