Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi,George Mwakajinga akionyesha silaha iliyokutwa kwa majambazi hayo.
Hawa ndio watu wanaoshikiliwa na Polisi,baada ya kujeruhiwa na wananchi wenye hasira kali.
Jeshi la Polisi Mkoani Lindi linawashikilia watu wawili kwa Tuhuma za
Unyanganyi kwa kutumia silaha na kujeruhi Mfanyabiasha wa Duka katika
kijiji Cha Kitomanga Wilayani Lindi huku wakiwa katika hospital ya
Mkoa baada ya kunusurika kufa kufuatia Wananchi wenye hasira kutaka
kuwaua kwa kuwachoma Moto.
Akiongea na waandishi wa habari Ofisi kwake hii leo,Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Lindi,George Mwakajinga alieleza kuwa Watuhumiwa hao
waliojitambulisha kwa Rajabu Juma Mbete(26) mkazi wa manispaa ya Lindi
na Hamis Athuman(32) mkazi wa Mbembetini Kibiti Mkoani Pwani licha ya
kupora simu 6 na fedha taslim laki 6 pia walimjeruhi kwa Mapanga Bw
Hamis Hassan Muuza duka hilo.
Mwakajinga alibainisha kuwa Majambazi hayo yanayosadikiwa kuwa 4
walifanikiwa kukimbia baada ya Bunduki waliyokuwa nayo kugoma kufyetua
risasi hali iliyofanya wanavijiji vya Kitomanga,Mkwajuni na Mbwemkuru
kuanza msako na kufanikiwa kuwakamata na kuwajeruhi kwa kuwapiga na
kuwachoma moto kabla hawajapata msaada wa Jeshi la Polisi.
Akielezea kuhusu kukutwa na risasi tatu za Shortgun,Bangi pamoja na
Bunduki aina ya Shortgun ya kienyeji, Kamanda mwakajinga alifafanua
Bunduki hiyo Ambayo hutumia risasi za Short gun pia walikutwa na
risasi 3.
Kufuatia kukamatwa kwa majambazi hao baadhi ya Wafanyabiashara
Manispaa ya Lindi akiwemo Seif Nasor na Ahmaid Nachuli wameeleza kuwa
tatizo la kuongezeka kwa majambazi kunachangiwa na Uozo wa sheria hali
inayosababisha jamii kujichulia sheria mkononi.
Watuhumiwa hao ambao wamelazwa huku wakiwa chini ya Ulinzi wa Jeshi
la Polisi watafikishwa mhakamani mara baada ya Afya yao Kuimarika
kutokana kunusurika kuchomwa Moto na Wananchi ambapo tayari wameweza
kutambuliwa na baadhi ya wanakijiji
PICHA NA MICHUZI BLOG
PICHA NA MICHUZI BLOG
0 comments:
Post a Comment