na Mwandishi wetu, Lindi
MKUU
wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila, ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) kujikita zaidi kwenye uhamasishaji zaidi hususan maeneo ya vijijini
ambako mahitaji ya huduma za afya kwa wananchi walio wengi yako huko.
Mwananzila
alitoa ushauri huo kwenye maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili ambayo kitaifa
yamefanyika mkoani hapa.
“…hakikisheni
kasi ya uhamasishaji inaongezeka na wanachi wengi wanajiunga kwenye mfuko huu.
Haiwezekani kwa Mkoa wa Lindi uwe na wanachama asilimia 5.4 ya kaya 194,424
,hii ni ishara tosha kuwa wananchi hawajapata elimu ya dhana na umuhimu wa
mfuko huu,” alisema mkuu huyo wa mkoa ambaye alimwakilisha Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii kwenye maadhimisho hayo.
Ameutaka
mfuko huo kujipanga vema kukabiliana na changamoto za huduma za matibabu
zilizopo kwenye mkoa huo hususan uhaba wa dawa katika vituo vya matibabu.
Mwakilishi
wa NHIF Ofisi ya Mkoa wa Lindi, Fortunata Kulaya, alisema changamoto kubwa iko
kwenye matumizi ya fedha za tele kwa tele na zinazolipwa na MHIF kutokutumiwa
kwa malengo yaliyokusudiwa, hivyo kudhoofisha mwitikio wa wananchi kujiunga na
Mifuko ya Afya ya Jamii (CHF).
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment