Home » » Vijiji vya Litama,Nachinyimba,Chilangalile na Michenga Wilayani Ruangwa, wakabithiwa Ma Trekta!

Vijiji vya Litama,Nachinyimba,Chilangalile na Michenga Wilayani Ruangwa, wakabithiwa Ma Trekta!  Trekta 4 zilizonunuliwa kupitia Mpango wa kuendeleza kilimo wilayani(DADPS) Kabla ya kukadhiwa kwa

vijiji vya  Litama,Nachinyimba,Chilangalile na Michenga Wilayani Ruangwa

 .Mkurugenzi  mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw Reubern Mfune akiweka saini mkataba wa makabidhiano na Mwenyekiti wa kijiji cha kijiji cha Nachinyimba Bw Hassan Saidi Mchaka 
 .Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Bi Agness Hokororo(Mb) akijaribu kabla ya kukabidhi trekta na mkataba wa umiliki wa Trekta hiyo kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Chilangalile kata ya Makanjiro,Bw Juma saidi Nangolingo huku ikishuhudiwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw Reubern Mfune katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika mbele ya ofisi ya Idara ya Kilimo Wilayani Ruangwa
Wananchi wakishuhudia makabidhiano hayo. 

Picha na habhari na Abdulaziz Video, Ruangwa

 Jumla ya hekta 14960 zinatarajiwa kulimwa wilayani Ruangwa  Msimu huu wa kilimo 2012/13 kufuatia upatikananji wa matrekta makubwa yaliyotolewa na Halmashauri hiyo  na kukabidhiwa kwa vijiji Vinne vilivyopo Wilayani Humo.

Hayo yalielezwa na Mkuu wa wilaya ya Ruangwa,Bi Agness Hokororo(Mb)alipokuwa akikabidhi trekta 4 aina ya  Farmtrac (70E 60 HP 2WD)zilizonunuliwa Kupitia  Mpango wa Maendeleo na Uendelezaji Kilimo wilayani(DADPS)Yenye thamani ya Tshs 160 Milioni ikiwa ni gharama ya Ununuzi na Usafirishaji hadi kufika wilayani humo.
Akiongea na Wakulima hao baada ya Taarifa fupi ya makabidhiano iliyosomwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw Reubern Mfune,Mkuu wa wilaya aliwataka wakulima hao kuanzisha akaunti maalum

ya kuyatunza matrekta hayo na mapato yote kuwekwa katika akaunti hizo ili kusaidia kumudu kujiendesha ikiwa pamoja na kuchangia asilimia 20 kwa ajili ya marejesho ya ununuzi wa trekta hizo ili kijiji kiweze
kumilikishwa.

Aidha Bi Hokororo aliitaka halmashauri hiyo kupitia maafisa Ugani kuhakikisha wanasaidia uendeshaji wa miradi hiyo huku wakiamasisha Jamii kuandaa mashamba yao ili yasiwe na Visiki ikiwa pamoja na kuhakikisha trekta hizo zinabeba mzigo uliolingana na uwezo uliopangwa kubebwa na trekta hizo.

‘’Nataka muhakikishe kuwa trekta hizo ninazowakabidhi leo zinatumika kwa misingi ya kilimo na ziendeshwe na dereva mwenye leseni na aliepatiwa Mafunzo na si Vinginevyo’’’Alimalizia Hokororo.

Vijiji vilivyonufaika na Mpango huo ni Litama,Nachinyimba,Chilangalile na Michenga ambazo ziliwezeshwa kuibua miradi ya Kilimo na kupatiwa

Mafunzo
0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa