Eneo la tukio
Ingawa vifaa vilikuwa duni kazi ya uokoaji iliendelea
Watu walifanya kazi kufa na kupona
Baadhi ya maiti akitolewa eneo la tukio
Mbunge wa Ruangwa Mh. Kassim Majaliwa akiwa eneo la tukio sambamba na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Agness Hokororo
RPC wa Lindi MWAKAJINGA na OCD wa RUNGWA V.P MAJANI wakitoa pole kwa wafiwa na shukrani kwa waokoaji
Maafa makubwa yametokea jana katika kijiji cha Mnacho maeneo ya Nandagala wilayani Ruangwa (pichani) baada ya wachimba madini saba kufukiwa na kifusi cha mwamba. Kazi ya uokozi ilianza jana majira saa 9 jioni na imechukua masaa zaidi ya 12 kutokana na uduni wa vifaa vya uokoaji. Katika tukio hilo watu saba wamepotea maisha na miili yote imepatikana . Majina ya Marehemu wa kadhia hiyo ni Chakoda - 20 mkazi wa Dar es salaam, Nyang'ana - 42 mkazi wa Musoma, Uwesu Bakari - 25 mkazi wa Rondo Lindi, Mohamedi Omary - 28 mkazi wa Morogoro, Bakari Rashidi Liganga - 26 mkazi Chunyu Ruangwa, Adam Sayai Mkazi wa bunda na Rashid Hamis Yasin wa Nachingwea
0 comments:
Post a Comment