Home » » UOKOAJI MAITI ZILIZOFUKIWA NA KIFUSI RUANGWA WAKAMILIKA

UOKOAJI MAITI ZILIZOFUKIWA NA KIFUSI RUANGWA WAKAMILIKA

Maiti za wachimbaji wadogo wa Madini katika Machimbo ya Madini katika Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa Mkoani Lindizikiwa zimetolewa tayari kwa utambuzi. Watu saba walifukiwa na Kifusi na kupoteza maisha katika moja ya Mashimo ya Mgodi huo juzi.
Zoezi la uokoaji lililokuwa likifanywa na wananchi wa Kata ya Ndagala yalipo Machimbo ya Madini katika Kata hiyo Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi ukiendelea.Kikosi cha wananchi cha Uokoaji kikiwa kimewafikia watu hao waliofukiwa na kifusi.
Na Abdulaziz video
Zoezi la kufukua Maiti za watu waliofunikwa na kifusi katika Machimbo ya Madini katika Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi jana limekamilika leo asubuhi huku wakifanikiwa kuzipata maiti zote 7

Akiongea na mtandao huu,Diwani wa Kata hiyo,Andrew Chikongwe alibainisha kuwa kazi ya kufukua kifusi hicho imechukua muda mrefu kufuatia na kuwepo kwa zana duni za kufukua Mchanga hali iliyofanya kazi hiyo kuwa Ngumu kuanzia jana saa 9 jioni hadi leo asubuhi

Chikongwe aliwataja Marehemu hao ni Nyang'ana Mkelecha,Mkazi wa Musoma,Mohamed Omari Fondogoro,Mkazi wa Morogoro,Bakari Liganga mkazi wa Chunyu Ruangwa,Rajab maarufu ROGER Mkazi wa Musoma,Uwesu Bakari Abeid mkazi wa Rondo,Chakoda Mkazi wa Dar na Rashid Ally maarufu BADE Mkazi wa Masasi mkoani Mtwara
Chanzo: Mrokim blog

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa