Home » » BIL 3.3/- KUSAMBAZA UMEME LINDI

BIL 3.3/- KUSAMBAZA UMEME LINDI

JIBU LA SWALI LA MBUNGE Mchinga

na Mwandishi wetu, Dodoma
SERIKALI ilitenga kiasi sh bilioni 3.3 kwa ajili ya kusambaza umeme katika mkoa wa Lindi kwa kipindi cha mwaka 2011/12.
Hayo yalielezwa jana bungeni na Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, George Simbachawene kwa kueleza kuwa fedha hizo zilitolewa katika mpango wa serikali wa kusambaza umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Simbachawene alieleza hayo wakati alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Mchinga, Saidi Mtanda (CCM).
Mbunge huyo alitaka kujua ni kiasi gani cha fedha kilitengwa katika kukamilisha miradi ya usambazaji umeme mkoa wa Lindi.
Pia Mtanda alihoji ni lini maeneo ya vijiji vya Rutamba, Milolo, Kitange, Kitomanga, Mipingo na Kilolambwani yatapatiwa umeme na kiasi cha fedha kitatumika.
Mbali na hilo, alitaka serikali itoe tamko lini itawalipa fidia wananchi waliohama katika maeneo yao kupisha miradi hiyo.
Akitoa ufafanuzi wa swali hilo alisema kuwa fedha zilizotengwa zinahusisha maeneo ya wilaya ya Ruangwa Vijijini, Kiwanja cha Ndega cha Lindi, Kijiji cha Dodoma, kilichopo wilayani Ruangwa na eneo la Ugogoni B na Mianzini Voda wilayani Nachingwea.
Kuhusu usambazaji wa umeme katika vijiji vya Rutamba, Milola, Kilangala, Kitomanga, Mpigo na Kilolambwani, Naibu Waziri, alisema mradi wa umeme katika maeneo hayo utaanza kutekelezwa katika mwaka wa fedha wa 2013/14.
Alizitaja gharama zitakazotumika kwa ajili ya mradi huo kuwa ni shilingi bil. 5 ambazo zitatolewa na Wakala wa Nishati Vijijini REA.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa