WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amepokea wanachama wapya 37 kutoka vyama vya CUF
na CHADEMA ambao wameamua kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM).
Kwa mujibu wa Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Bw. Barnabas Essau wanachama 35 kati ya hao wametoka CUF na wawili wametoka CHADEMA.Wanachama
hao walipokelewa jana (Jumapili, Novemba 5, 2017) kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika kijiji cha Mbekenyera, wilayani Ruangwa mkoani
Lindi.
Bw.
Essau alisema wanachama hao wote wametoka kata za Mbekenyela na
Matambalale. Walikabidhiwa kadi mpya za CCM, na kula kiapo cha uaminifu.
Akizungumza
kwa niaba ya wanachama wenzake wapya, Bw. Mohammed Issa Ndogoro ambaye
amehamia kutoka CHADEMA, alisema wamejiunga na CCM baada ya kuridhishwa
na mwelekeo wake. Alisema wameguswa na jinsi Serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli inavyofanya kazi ya kutatua kero
za wananchi.
Alisema
amekaa upinzani kwa miaka 23 lakini anaikubali CCM sababu ya uwazi wake
na ameshangaa kuona akipewa kadi na stakabadhi ya walipo yenye jina
lake, jambo ambalo hajawahi kuliona katika vyama vingine vya upinzani.
“Sote
sisi tumehamia CCM, uhai wa chama ni michango. Nani aseme hapa kama
aliwahi kupewa stakabadhi katika chama chake, na kama yupo nampa sh.
5,000/- sasa hivi,” alisema Bw. Ndogoro na kuamsha kicheko kwenye
mkutano huo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
40480 - DODOMA.
JUMATATU, NOVEMBA 6, 2017.
0 comments:
Post a Comment