LINDI:
 Manispaa ya Lindi imepata Gawio la Zaidi ya  Sh 1.9 Bilioni kutojana na
 uwekezaji wa pamoja na Upimaji wa viwanja kwa kushirikiana na taasisi 
ya Uwekezaji Tanzania (UTT-PID).
Akielezza
 Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ya Lindi, Bw. Jomaary Satura wakati wa 
kikao cha kuangalia mafanikio kilichofanyika jana, ambapo alibainisha 
kuwa,  fedha hizo  ni mafanikio ya upimaji  wa viwanja  2,500 kati ya 
10,000 walivyokusudia  kupima awamu ya kwanza.
“Fedha
 hizi zimetumika kujenga miradi mbalimbali kwenye Manispaa yetu. Ikiwemo
 kujenga Maabara na vifaa vyake, Ujenzi wa Zahanati, Nyumba ya Mganga na
 Boti ya kisasa.” Alieleza Mkurugenzi huyo.
Aidha
 aliongeza kuwa, mapato ya ndani ya ndani kwa sasa yameongezeka kwa 
kupanda kutoka  Sh 700 Milioni  mwaka 2013 hadi Sh 2.4 Bilioni.
Kwa
 upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya UTT-PID, Bi. Janet Mmari amesema 
mradi huo umegharimu Sh.1.9 Bilioni hivyo umeonyesha mafaniko kwa jamii.
“Mradi huu ulikuwa ni wa gawio la asilimia 50 kwa 50. Tunawapongeza Manispaa kwa kufanya kazi vizuri” alisema Bi. Janet Mmari.
Naye
 Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alisema kuwa, awamu ya pili 
watashirikisha makundi yote ikiwemo wanasiasa ilikuondoa mivutano 
inayosababisha kuchelewa kwa maendeleo.
“Maendeleo
 yanapatikana mawazo yanapogangana. Nyingine ni changamoto za kawaida na
 uelewa, Wanasiasa kuingilia kunatokana na masilahi binafsi” alieleza 
Mkuu wa Mkoa huyo.
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment