Na Tiganya Vincent-MAELEZO
Wizara
ya Maliasili na Utalii imesema kuwa inatarajia kuboresha utalii wa
kusini mwa Tanzania kupitia miradi mbalimbali kwa kushirikiana na wadau
wa maendeleo chini ya mradi wa REGROW unaofadhiliwa na Benki ya Dunia
kwa gharama za shilingi bilioni 2.1.
Fedha hizo zinafadhiliwa na Benki ya Dunia sawa na Dola za Kimarekani zisizopungua milioni moja.
Kauli
hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Injinia Ramo Makani wakati akijibu swali Mbunge wa Jimbo la Lindi
Mjini Mhe. Hassan Kaunje aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa
kuendeleza utalii wa ukanda wa kusini.
Alisema
kuwa hatua hiyo inalenga kuwekeza katika miundombinu ya utalii kwa
ajili ya kuutangaza utalii wa Ukanda wa Kusini mwa Tanzania ili uweze
kusaidia ukuaji wa uchumi na ustawi wa Taifa.
Alisema
kuwa mpango huo utajumuisha kuimarisha mafunzo ya utalii na kutenga
maeneo maaalum ya utalii katika fukwe za bahari na maziwa kwa ajili
hoteli za kitalii.
Mhe.
Makani alisema kuwa Serikali imepanga kutekeleza mkakati wa kuutangaza
maeneo ya utalii ikiwemo vivutio kihistoria na kiutamaduni kama vile mji
wa kihistoria wa Mikindani, Kilwa Kivinje, Pori la Akiba Lukwika-Lumese
na Pori la Akiba la Seleous.
Aliongeza
kuwa ili kukuza utalii wa fukwe katika eneo hilo , Serikalai imejipanga
kutenga maeneo maalum hususan kwa ajili ya hoteli za kitalii kando ya
Bahari ya Hindi mkoani Mtwara na Lindi.
0 comments:
Post a Comment