Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Chama
 cha Ushirika (NANYUM) wilayani Lindi kitatakiwa kulipa deni la sh. 
milioni 433 kwa wakulima wa korosho wilayani humo baada ya kukamilika 
kwa uchunguzi wa tukio la wizi wa fedha hizo lililodaiwa kufanyika 
Januari, mwaka huu.
Katika
 taarifa iliyotolewa leo (Mei 12,2016) na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi
 inasema kutokana na tukio lililotokea mnamo Januari 7, mwaka huu majira
 ya saa 12:30 za jioni huko kijiji cha Nambahu majambazi wapatao watatu 
wakiwa na bunduki huku wakitumia usafiri wa pikipiki walivamia Ofisi ya 
NANYUM na kupora pesa taslimu sh. milioni 433.
Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa siku ya tukio hilo, kiasi cha fedha hizo zilichukuliwa kutoka Benki ya  NMB
 ya Lindi Mjini zikisindikizwa na polisi hadi kijijini Nambahu wakiwa na
 viongozi wa chama hicho Bw. Mohamedi Chilumba na Bw.Hassani Mundedu na 
fedha hizo zilikabidhiwa na kupokelewa na chama kupitia vitabu vya 
mahesabu.
“Baada
 ya kupata taarifa ya tukio kutoka kituo cha polisi Tandahimba, polisi 
walikwenda kijiji hapo majira ya saa 4:30 usiku na kuchukua maelezo ya 
viongozi tisa wa NANYUM juu ya tukio hilo ambapo walitaka kupewa taarifa
 kama  kulisalia
 kiasi chochote cha fedha baada ya tukio.Lakini viongozi hao wote 
walikana kwamba hakuna hata kiasi kilichobakia” ilieleza taarifa hiyo.
Aidha
 taarifa hiyo ilifafanua kwamba katika uchunguzi wa polisi ulibaini kati
 ya sh. milioni 443 zilizokabidhiwa kwenye chama hicho kutoka benki ya 
NMB tawi la Lindi hazikuibiwa zote. Hivyo baada ya wajumbe wa bodi hiyo 
kuhojiwa na polisi jumla ya sh. milioni 32 zilipatikana. Hadi sasa 
baadhi ya wajumbe hao wanashikiliwa na polisi ili kubaini upotevu wa 
fedha hizo.
Taarifa
 hiyo ilieleza kwamba kama itathibitika kisheria kwamba viongozi wa 
chama hicho wamehusika katika tukio hilo na kupatikana na hatia ya wizi 
watalazimika kulipa fedha hizo na Serikali itaendelea kufuatilia matukio
 kama hayo na kuhakikisha kwamba wakulima wanapata haki zao.
 

 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment