Home » » Huawei yaendelea kusaidia Sekta ya Afya na Elimu nchini

Huawei yaendelea kusaidia Sekta ya Afya na Elimu nchini

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (Kulia) akiangalia ramani ya Zahanati na Nyumba ya wafanyakazi mara baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Bw. Bruce Zhang kutoa msaada wa kompyuta 25 na UPS 25 kwa shule tano za sekondari pamoja na kuzindua ujenzi wa mradi wa Zahanati ya kijiji cha Nandagala wilayani ya Ruangwa utakaojengwa na Kampuni hiyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (Kushoto) akimpongeza mkutugenzi mtendaji wa kampuni ya Huawei Tanzania Bw. Bruce Zhang (Katikati) mara baada ya Kampuni hiyo kutoa msaada wa kompyuta 25 na UPS 25 kwa shule tano za sekondari pamoja na kuzindua ujenzi wa mradi wa Zahanati ya kijiji cha Nandagala wilayani ya Ruangwa utakaojengwa na Kampuni hiyo.

Teknolojia ya Habari na Mawasiliano imekua kuanzia katika utangazaji kwa njia ya televisheni hadi matumizi ya simu za mikononi na sasa matumizi ya intenet yameibadilisha dunia kwa kiasi kikubwa.

Kwa watu wengi ni ngumu kufikiria jinsi maisha yangeweza kuwa rahisi kwa kiasi hiki, ukuaji wa huduma ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) umesaidia kurahisisha maisha.

Wakati wengi wakiendelea kufurahia fursa zilizotokana na kukua kwa teknolojia, kuna kundi la watu zaidi ya bilioni ambao wameachwa nyuma kwa sababu mbali mbali. Ukuaji wa TEHAMA umeleta mgawanyiko wa kiteknolojia kwa watu.

Kama kiongozi  katika teknolojia ya habari na mawasiliano, kampuni ya Huawei imekuwa kinara katika kutoa mifumo bora ya TEHAMA, vifaa pamoja na utaalam wa teknolojia ili kuondoa mgawanyiko huo uliopo katika dunia.

Kampuni hii imelenga kuunganisha jamii ambayo bado haijaunganishwa, kuendeleza taaluma ya TEHAMA na kutoa ujuzi kwa wabunifu wanao chipukia na kuongeza thamani ya watumiaji kwa huduma hii.

Teknolojia ya Habari na Mawasiliano imeweza kuongeza uwajibikaji na uzalishaji kwa kuwezesha kuboresha sekta ya elimu na afya kwa watanzania, kupitia kampuni ya Huawei sekta hizi zimeweza kuendelea kukua kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanya na kampuni hii.

Kama kampuni kiongozi katika sekta ya mawasiliano duniani, mahusiano ya Huawei na serikali ya Tanzania katika masuala ya teknolojia yameanza muda mrefu tangu mwaka 2001.

Kwa miaka kadhaa sasa, kampuni ya Huawei imeshrikiana na serikali ya Tanzania, taasisi binafsi na makampuni binafsi kuwezesha ukuaji wa sekta ya mawasiliano nchini pamoja na kuboresha miundombinu ya TEHAMA.

Kwa sasa, Huawei imejidhatiti kuboresha maisha ya watanzania kupitia sekta ya mawasiliano, kuunganisha kundi la watanzania ambao bado hawajaweza kufurahia ukuaji wa sekta hii na mipango hiyo imeanza kuzaa matunga tangu kampuni hii ilipoanzisha huduma zake nchini mwaka 2001. 

Toka waka 2001, Huawei imetoa ajira nyingi kwa watanzania wengi, na kwa sasa kampuni hii imeweza kuajiri zaidi ya watu 230, ambapo kati yao 155 ni watanzania na  75 niwafanyakazi wenye uraia wa China na nchi nyingine, hivyo kufanya idadi ya watanzania kuwa asilimia 67.

Mchango wa Huawei kwa zaidi ya miaka kumi na tano iliyopita umeongezeka kwa kiasi kikubwa ambapo moja ya mipango hiyo ni kusaidia serikali ya Tanzania katika utekelezaji wa mkongo wa Taifa (NICTBB).

Akizungumza wakati wa utoaji wa misaada ya kompyuta 25 na UPS 25 kwa shule tano za sekondari na kuzindua ujenzi wa Zahanati ya Nandagala, wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, mkurugenzi wa Huawei Tanzania Bw. Bruce Zhang alisema kuwa kampuni hiyo imefanya mambo mengi katika kusaidia jamii ikiwemo kutoa misaada kwa taasisi za elimu ya juu, shule na hospitali na kurudisha fadhila kwa jamii.

Alisema kuwa, kwa miaka 15 ya utendaji kazi nchini, Huawei imetoa msaada wa kompyuta 100 na nguo  za michezo 4,000 kwa taasisi ya WAMA foundation inayoongozwa na mke wa Rais Mstaafu Dk Jakaya Mrisho Kikwete.

“Tumetoa pia vifaa mbali mbali kwa shule 10 za mikoani ikiwemo shule ya msingi Kakuni iliyoko mkoani Katavi, tumetoa mafunzo ya TEHAMA kwa watanzania zaidi ya 2,000 na pia msaada wa kifedha kwa miaka mitatu kwa chuo kikuu cha Nelson Mandera,” alisema.

Bruce alisema kuwa mwaka jana, kampuni hiyo ilishirikiana na serikali kuandaa kongamano la Huawei Cloud Congress (HCC) na Connect to Connect (C2C), na pia ilichangia ufanikishaji wa mkutano wa watanzania wanaoishi nje ya Tanzania mkutano uliofanyika ofisi za waziri mkuu.  

Anasema kuwa kwa kushirikiana na serikali, mwaka jana walisaini makubaliano ya pamoja katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ambapo kampuni hii ilipewa dhamana ya kuwa mshauri mkuu wa masuaila ya TEHAMA kwa serikali.

“Kupitia makubaliano hayo, Huawei itaendelea kufanya kazi na serikali kuboresha mifumo ya TEHAMA na pia kutunga sera, mafunzo, na kuendesha miradi mbali mbali ya kiteknolojia nchini,” alisema.

Aliongeza kuwa kampuni yake imetambuliwa mchango wake kwa serikali  ambapo mwaka jana ilizawadiwa hati kwa kutambua mchango wake kama kampuni iliyo mstari wa mbele katika maendeleo ya teknolojia nchini.

Bruce anasema kampuni yake imewekeza katika teknolojia kwa kuwawezesha vijana wa wakitanzania kupata uzoefu, na kuleta mabadiliko chanya ya katika teknolojia ya habari na mawasiliano.

Alisema mbali na kutoa vifaa vya teknolojia ya habari na mawasiliano Huawei imekuwa mdau mkubwa katika ujenzi wa mkongo wa taifa na kusaidia katika miladi ya elimu kwa njia ya kielektroniki.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo katika kijiji cha Nandagala, wilaya ya Ruangwa, Waziri mkuu Kassim Majaliwa alipongeza uamuzi wa kampuni hiyo kusaidia jamii ambayo ilikuwa ikikabiliwa na changamoto mbali mbali.

Alisema kuwa wakazi wa wilaya ya Ruangwa walikuwa na changamoto mbali mbali za ikiwemo utoaji wa mafunzo ya vitendo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa wanafunzi wa sekondari na pia kukosekana kwa huduma muhimu za kijamii ikiwemo afya.

Waziri Mkuu alishukuru kampuni hiyo na kusema kuwa kompyuta hizo ni muhimu kusaidia shule za sekondari  kufundisha wanafunzi kwa vitendo ili waweze kuendana na ukuaji wa teknolojia.

Alisema kuwa Tanzania itaendelea kujenga mahusiano na serikali ya China pamoja na makampuni kutoka nchini humo hasa katika sekta ya teknolojia ya habari na  mawasiliano kwa kuwa sasa serikali imeingia mkataba na kampuni ya Huaweei kama mshauri mkuu wa masuala ya Tehama.

“Tunashauri makampuni mengine ambayo yamewekeza Tanzania kuwa na mikakati ya kusaidia jamii, kwa kuonyesha nia yao njema kwa wananchi wanao wahudumia ili kuwezesha biashara zao kukua na kuleta imani kwa wananchi,” alisema.

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa