Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Baadhi ya madiwani na wafanyabiashara wa mazao ya misitu Wilayani Nachingwea mkoani Lindi, wamelalamikia urasimu wa utoaji wa vibali vya kusafirishia mazao ya misitu, unaofanywa na wakala wa huduma za misitu(TFS) unaosababisha wafanyabisha wa mazao ya misitu kukwepa kwenda vijijini kununua na kuvuna mazao ya misitu.
Madiwani na wafanyabiashara hao, waliyasema hayo kwenye kikao cha mrejesho wa mchakato wa uwajibikaji wa jamii katika usimamizi wa misitu, kilichoendeshwa na kuandaliwa na shirika lisilo la kiserika la jukwaa la sera (Policy forum) kwa ufadhili wa kampeni ya mama misitu, kilichofanyika jana, mjini Nachingwea.
Walisema kumekuwa na urasimu mkubwa unaofanya na wakala huduma za misitu katika utoaji wa vibali vya kusafirishia kwa wafanyabiashara. Hali inayosababisha wafanyabiashara kukwepa kwenda vijijini kununua na kuvuna mazao ya misitu na kusababisha soko la mazao kuwa gumu.
Mfanyabiashara, Polycap Cassian alisema kutokana na urasimu uliopo wakupata vibali vya kusafirishia, wafanyabiashara wanaogopa kwenda vijijini kuvuna na kununua mazao ya misitu. Hivyo wananchi ambao walikuwa na matarajio ya kunufaika na misitu wanakata tamaa.
Alisema kuna mzunguko mrefu wa kupata vibali vya kusafirishia, ambao unasababisha wapoteze muda mwingi wa kufanyabiashara. Hivyo alishauri vijiji vipewe uwezo wa kutoa vibali vya kusafirishia.
Diwani wa kata ya Mkotokuyana, Sada Makota, licha ya kulaumu urasimu katika utoaji wa vibali hivyo, lakini pia alilaumu mamlaka hiyo kugonga na kuweka alama zinazoruhusu kusafirishwa mbao zilizopasuliwa kwa kutumia misumeno ya moto(chain saw).
"Ingawa halmashauri imewaagiza maofisa wake wa idara ya maliasili kutogonga mbao zilichanwa kwa chenisoo lakini wenzetu wanazigonga na kuziruhusu zisafirishwe,"alisema Saada.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Ahmad Makoroganya, alisema ingawa wamekuwa wakitoa maagizo kwa maofisa waliochini ya halmashauri kutozigonga mbao zilizopasuliwa kwa misumeno hiyo, lakini imekuwa ni vigumu kudhibiti uvunaji unaotumia mashine ya hizo.
Kwamadai kuwa maagizo hayo yanaishia na kutekelezwa na maofisa hao waliochini halmashauri, wakati maofisa wa wakala huduma za misitu wazigonga na kuzipitisha.
Alisema hakukuwa na sababu ya wilaya kuwa na mameneja wa wakala wa misitu wakati kunamaofisa wa misitu wa wilaya.
"wakati misitu ipo ndani ya vijiji, wanatuletea meneja wasio wajibika kwetu" turejeshewe mamlaka kamili kwenye misitu, maana kunakitu hapa pembeni kinatuangusha,"alisisitiza Makoroganya.
Ofisa misitu wa Wilaya ya Nachingwea, Paiton Kamnana, alisema ingawa sheria inasema ofisi za idara za misitu inaweza kutoa vibali hivyo, lakini utekelezaji wake bado kufanyika na wizara ya maliasili na utalii.
Alishauri kuwepo mawasiliano ya mara kwa mara baina ya Halmashauri ya Wilaya na ofisi ya kanda ya wakala wa huduma za misitu kwani dhamira na malengo ni ya aina moja ambayo ni kuona jamii na taifa linanufaika na maliasili zilizopo nchini.
Alishauri kuwepo mawasiliano ya mara kwa mara baina ya Halmashauri ya Wilaya na ofisi ya kanda ya wakala wa huduma za misitu kwani dhamira na malengo ni ya aina moja ambayo ni kuona jamii na taifa linanufaika na maliasili zilizopo nchini.
0 comments:
Post a Comment