Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Jordan Rugimbana kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto amezindua rasmi kampeni ya kitaifa ya uhamasishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii ( CHF) katika kata ya Nyangamara iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Lindi akikabidhi kadi ya CHF kwa mnufaika mpya wa CHF Bw. Hassan Namangaya wakati wa Uzinduzi.
Mwenyekiti
wa CCM wa Lindi Mzee Mtopwa alihamasika na kuchangia kaya 8 za
wasiojiweza ili waandikishwe kwenye CHF. Aliesimama naye ni Mkuu wa
Wilaya ya Lindi Mh. Nawanda.
Wananchi wa Kata ya Nyangamara wakifuatilia Hotuba ya Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Katika
uzinduzi huo ulioratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa
kushirikiana na Halmashauri ya Lindi Vijijini kaya zipatazo 261(sawa na
wanufaika 1,566) zilisajiliwa papo hapo katika CHF kwa mchango wa
Shilingi 10,000 kwa mwaka. Pia Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Nawanda
alihamasisha viongozi mbalimbali wa Mkoa huo ambao hawakuwepo ambapo
zilichangwa fedha kwa ajili ya kaya 2,060 za watu wasio na uwezo ili
waandikishwe katika CHF.
Katika
uchangiaji huo Mh. Waziri Mkuu ambaye ni Mbunge wa Ruangwa alichangia
usajili wa kaya 900 ambapo Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh. Rugimbana
alichangia kaya 100, RAS Lindi - kaya 100, DC Lindi - kaya 50, NHIF kaya
300, Mh. Waziri wa Habari na Mbunge wa Mtama - kaya 300, Mh. Lalinda
Mbunge wa Viti maalum CUF - kaya 50, Mh. Hamida viti maalum CCM - kaya
60, Mh. Hamid Bohali Mbunge wa Mchinga - kaya 100, Mh. Kaunje Mbunge wa
Lindi - kaya 100.
Pia alihimiza makundi maalum ya wazee, yatima na wasiojiweza yatafutwe na kuchangiwa fedha ili wajiunge na CHF. Ali kufanikisha CHF, aliwahimiza wananchi kuwa huru kuwasilisha malamiko yao kwa uongozi ili yaweze kufanyiwa kazi. Akikamilisha uzinduzi huo alikabidhi mashuka 300 kwa wakuu wa wilaya yaliyotolewa na NHIF kwa ajili ya vituo vya afya katika mkoa wa Lindi lakini pia alikabidhi kadi za CHF kwa wanachama wapya wa CHF.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa CHF Bw. E. Mikongoti alisema mkoa wa LIndi
una wanufaika 89,836 wa CHF ambayo ni asilimia 6.6 ya wana Lindi.
Alihimiza Mkoa kuifanya CHF kuwa agenda katika utekelezaji mkoani hapo
lakini pia kutumia vema fedha za uchangiaji ili kuboresha huduma za afya
ili kuvutia wengi zaidi kujiunga na Mfuko huo.
Wakati
akiwasilisha ripoti ya CHF mkoa wa Lindi, Mganga Mkuu wa mkoa Dk. Sonda
alisema Lindi imefanikiwa kupata malipo ya Tele kwa Tele ya CHF ya
SHilingi 109,436,000 kwa mwaka 2015 ambazo ni mchangi mkubwa katika
kuboresha afya mkoani humo. Hata hivyo aligusia kusema bado wana
changamoto ya hamasa ya watendaji kuhusu CHF.
Kwa
upande wake Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Lindi ukizindua uhamasishaji
huo aliwahimiza wananchi kuona umuhimu wa kuchangia kiasi kidogo cha
fedha kwenye CHF ili wapate kadi ya matibabu kwa kaya kwa mwaka mzima.
Pia alitoa maagizo kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Wilaya za Lindi
kuwa kuanzia sasa ni mwisho kufanya matibabu kwa malipo ya papo kwa
papo na endapo mtu atalipa papo kwa papo basi alipishwe shilingi 10,000
kila anapoenda kupata matibabu. Alisema haiwezekani kwa mkoa wa Lindi
kuwa na asilimia chache hivyo za watu waliojiunga na CHF.
Pia alihimiza makundi maalum ya wazee, yatima na wasiojiweza yatafutwe na kuchangiwa fedha ili wajiunge na CHF. Ali kufanikisha CHF, aliwahimiza wananchi kuwa huru kuwasilisha malamiko yao kwa uongozi ili yaweze kufanyiwa kazi. Akikamilisha uzinduzi huo alikabidhi mashuka 300 kwa wakuu wa wilaya yaliyotolewa na NHIF kwa ajili ya vituo vya afya katika mkoa wa Lindi lakini pia alikabidhi kadi za CHF kwa wanachama wapya wa CHF.