Wananchi
wote mnakaribishwa kutembela banda la Wizara ya Fedha na taasisi zilizo
chini yake ikiwemo UTT AMIS, Mfuko wa Pensheni PPF, GPSA na UTT PID
uwanja wa maonesho ya kilimo ya Nane Nane Kitaifa Ngongo mkoani Lindi.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Josephat
Mwambega akipokea fomu ya kujiunga na Mfumo wa Amana inayotolewa na
Mfuko wa Pensheni wa PPF kutoka kwa Afisa Masoko wa Mfuko huo Nelusigwe
Mwalugaja wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha. Wa kwanza kulia
ni Mhasibu kutoka PPF.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Josephat
Mwambega akiongea na Afisa Msoko na Uhusiano, Rahimu Mwanga kutoka
taasisi ya UTT AMIS kwenye Uwanja wa maonesho ya Kilimo ya Nane Nane
Ngongo Mkoani Lindi.
Afisa
Masoko na Uhusiano, Rahimu Mwanga kutoka taasisi ya UTT AMIS akiongea
na baadhi ya wageni wakijionea kazi mbalimbali zinazofanywa na taasisi
hiyo wakati wa maonesho ya Kilimo ya Nane Nane uwanja wa Ngongo Mkoani
Lindi.
Mhasibu
kutoka Idara ya Pensheni Wizara ya Fedha, Imelda Mzatulla akiongea na
baadhi ya wageni waliofika kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa na
Wizara ya Fedha wakati wa maonesho ya Kilimo ya Nane Nane uwanja wa
Ngongo Mkoani Lindi.
Afisa
Masoko Mfuko wa Pensheni wa PPF, Nelusigwe Mwalugaja (kulia) akiongea
na Mkurugenzi wa Mafunzo ya Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na
Ushirika Anne Assenga (kushoto) wakati wa maonesho ya Kilimo ya Nane
Nane Kitaifa yanayoendelea uwanja wa Ngongo Mkoani Lindi.
Afisa
Masoko na Uhusiano wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu
(UTT PID), Kilave Atenaka akifafanua jambo kwa baadhi ya wageni
waliotembelea banda la taasisi hiyo wakati wa maonesho ya Kilimo ya Nane
Nane Kitaifa yanayoendelea uwanja wa Ngongo Mkoani Lindi.
Mtaalamu
wa Mawasiliano kutoka Program ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za
Umma (PFMRP) Wizara ya Fedha, Alexander Iweikiza akimsikiliza Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Josephat Mwambega
alipotembelea Banda la Wizara hiyo wakati wa maonesho ya Kilimo ya Nane
Nane Kitaifa yanayoendelea uwanja wa Ngongo Mkoani Lindi.
Mhasibu
kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anne Paul akiwapa zawadi wanafunzi wa
shule ya msingi Tulieni iliyopo kata ya Mnazi Mmoja walipotembelea banda
la maonesho mfuko huo wakati wa maonesho ya Kilimo ya Nane Nane Kitaifa
yanayoendelea uwanja wa Ngongo Mkoani Lindi.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya wageni waliofika banda la Wizara ya Fedha
kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa na Wizara ya Fedha na taasisi
zake.(Picha na Eleuteri Mangi- MAELEZO, Lindi).
0 comments:
Post a Comment