Home » » BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO (TADB) YAFANYA BONANZA LA NANENANE MKOANI LINDI‏

BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO (TADB) YAFANYA BONANZA LA NANENANE MKOANI LINDI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

1
Kaimu Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Bi. Miriam Mtima akizungumza wakati wa kufungua bonanza la Nanenane lilioandaliwa na benki ya Maendeleo ya Wakulima (TADB), jana mkoani Lindi.
2
Mkurugenzi wa Mikopo wa benki ya Maendeleo ya Wakulima, Bwana Robert Paschal akitoa hotuba ya ufunguzi wakati wa uzinduzi wa bonanza la Nanenane katika viwanja vya Ilulu mkoani Lindi jana.
4
Kaimu Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Bi Miriam Mtima akipiga mpira kuashiria ufunguzi wa bonanza la Nanenane lilioandaliwa na benki ya Maendeleo ya Wakulima (TADB), jana mkoani Lindi.
3
Vijana wakishiriki shindano la kuvuta kamba.
6
Vijana wakishiriki mashindano ya riadha.
7
Mashindano ya kukimbia na magunia.
5
Kikundi cha Ngoma na sarakasi cha Akoa Mpiluka kikitoa burudani.
Benki mpya ya Maendeleo ya Kilimo, leo imefanya bonanza maalumu la kuhamasisha wananchi kushiriki katika uzinduzi wa benki hiyo utakaofanyika katika kilele cha maonyesho ya Nanenane yanayoendelea hapa mkoani Lindi.
Katika bonanza hilo lililojumuisha michezo mbalimbali kama vile ngoma za jadi, muziki, mpira wa miguu na mpira wa pete kwa wanawake lilianza majira ya saa nane mchana na kukamilika saa kumi na mbili jioni.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Bi Miriam Mtima amewataka wakazi wa Lindi hasa vijana kujipanga kutumia fursa zitakazotolewa kupitia benki hiyo na kwamba ofisi yake iko tayari kushirikiana nao watakapoanzisha vikundi kwa ajili ya kujishughulisha na kilimo.
"Niwahamasishe tujitokeze kwa wingi tarehe nane, Rais atakuja kuizindua benki hii maalumu kabisa kwa wakulima ambayo itatoa fursa za mikopo kwa vijana watakaoungana kwa ajili ya shughuli za kilimo’ alisema Bi Mtima.
Awali katika hotuba ya kumkaribisha Mgeni Rasmi katika bonanza hilo, Mkurugenzi wa Mikopo wa benki, Bwana Robert Paschal amesema kuwa bonanza hilo ni mwanzo wa shughuli mbalimbali zitakazoendelea mkoani humo kama utangulizi wa shughuli kubwa ya uzinduzi.
"Bonanza hili la leo na matembezi ya hisani yatakayofanyika siku ya ijumaa ni mwendelezo wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na Benki ya wakulima ili kuwaandaa wananchi na hasa wakulima na wafugaji kushiriki kikamilifu katika uzinduzi wa benki yao siku ya jumamosi kwa malengo makuu mawili, kwanza waielewe nini hasa adhima ya serikali kuanzisha benki ya kilimo, baada ya kuilewa wajiandaye kutumia fursa zitakazoletwa na benki hii" alisema Robert Paschal.
Benki hiyo itakayofunguliwa rasimi kesho tarehe 7 jijini Dar es Salaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Mrisho Kikwete na baadae kuzinduliwa rasmi katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa mjini Lindi yakiwa na lengo la kuchochea maendeleo ya kilimo kwa kutoa mikopo kwa wakulima wadogo na wakati.

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa