Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Waziri
 wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akisalimiana 
na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi mara baada ya kuwasili 
mkoani humo kwa ziara ya siku mbili amapo atasikiliza na kutatua 
migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali yenye migogoro katika mkoa 
huo.
 Mkuu
 wa Mkoa wa Lindi Mama Mwantum Mahiza akitoa taarifa fupi ya utekelezaji
 wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika mkoa huo kwa Waziri wa Ardhi 
Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Mh William Lukuvi mara baada ya Waziri Lukuvi kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
 Waziri
 wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akijadiliana 
jambo na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mama Mwantum Mahiza muda mfupi baada ya 
Mama Mahiza kutoa taarifu fupi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya 
maendeleo mkoani humo
 Waziri
 wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akijadiliana 
jambo na Mkurugenzi wa shirika la nyumba la Taifa Mkoa wa Lindi Bw Mussa
 Patric Kamenda badaa ya mkurugenzi huyo kutoa taarifa kwa Mheshimiwa 
Waziri jinsi shirika hilo linanvyotekeleza miradi mbalimbali katika mkoa
 huo.
 Waziri
 wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi (kulia) 
akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mama Mwantum Mahiza (kushoto) 
kuhusu ujenzi wa nyumba unaofanywa na Shirika la nyumba la Taifa mkoani 
Lindi. Katikati ni mfanyabiashara wa mkoa wa Lindi Bw Kassim Abdallah 
ambaye amenunua mojawapo nyumba ambazo zimejengwa na shirika la nyumba 
la Taifa.
Waziri
 wa ArdhiNyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akitoa 
malelekezo kwa Bwana Mussa Patric Kamenda Mkurugenzi wa shirika la 
nyumba la Taifa Mkoa wa Lindi   namna bora ya kutumia viwanja kwa ujenzi wenye manufaa kwa kulunufaisha shirika hilo.
Picha na Clarence Nanyaro.
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment