Home » » Wateja wa viwanja Lindi waendelea kusaini hati jijini Dar e Salaam‏

Wateja wa viwanja Lindi waendelea kusaini hati jijini Dar e Salaam‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

iiiAfisa Ardhi wa Lindi anayeshughulikia hati hizo jijini Dar es Salaam Mpoki Daimon (katikati), akimpa maelezo mmoja wa wateja waliofika kwenye ofisi za UTT-PID, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya zoezi hilo la saini. Kushoto kwake ni Afisa wa UTT-PID ambao ndio wawezeshaji wakuu wa mradi huo, Martin Mchanjila.
Na Mwandishi Wetu
Wateja wa mradi wa Viwanja vilivyopo Manispaa ya Lindi wameendelea kusaini hati zao jijini Dar es Salaam kwa uratibu wa Manispaa ya Lindi kwa ushirikiano na Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyo chini ya Wizara ya Fedha (UTT-PID), ambao ndio wawezeshaji wakuu wa mradi huo.
Wateja hao wameendelea kujitokeza katika ofisi za UTT-PID zilizopo katikaati ya jiji katika jengo la Golden Jubilee Tower, ambapo zoezi hilo linaendelea.
Akielezea zoezi hilo kwa upande wa Afisa Ardhi wa Lindi anayeshughulikia hati hizo jijini Dar es Salaam Mpoki Daimon alibainisha kuwa wameendelea kusainisha wateja wao hao kila siku huku akiwataka pindi wanapofika kuwa na vitu muhimu vitavyowatambulisha.
“Kwa sasa tunaendelea kusainisha wateja wetu walioomba viwanja Manispaa ya Lindi. Ambapo pia tunawataka kufika na vitu muhimu ikiwemo cheti za kuzaliwa ama hati ya kusafiria au kadi mpiga kura ilikuwezesha kuingiza data muhumu katika saini za hati zao” alieleza afisa ardhi huyo, Mpoki Daimon.
Kwa upande wake, afisa wa UTT-PID ambao ndio wawezeshaji wakuu wa mradi huo, Martin Mchanjila anayeshughulikia zoezi hilo alieleza kuwa hadi sasa zaidi ya wateja 200, wamejitokeza kutia saini hati zao hizo na bado zoezi linaendelea hadi hapo watakapomaliza.
“Kwa sasa jumla ya viwanja 1356 kwa mikoa ya Lindi, Mtwara na Dar es Salaam, wateja waliolipia ndio wanasaini hati zao kupitia kila mkoa na kwa wa Dar wanasaini hati zao hizo hapa UTT-PID.” Alibainisha Martin Mchanjila.
Mbali na Dar es Salaam katika ofisi za UTT-PID, pia zoezi hilo la kutia saini hati hizo kwa wateja linaendelea Lindi na Mtwara.
u
Ofisa wa UTT-PID akitoa akiwapa maelezo wateja (waliokaa) walio0fika kwa ajili ya zoezi la utiaji saini hati za viwanja vyao linaloendelea katika ofisi za UTT-PID, jijini Dar e Salaam
wwAfisa wa UTT-PID ambao ndio wawezeshaji wakuu wa mradi huo, Martin Mchanjila (kushoto) akitoa akimpa maelezo mmoja wa wateja walifika kwenye zoezi hilo la utiaji saini, linaloendelea katika ofisi za UTT-PID jijni Dar es Salaam.
aqq
Maofisa wa UTT-PID na Afisa wa Ardhi, Lindi, Bw. Mpoki wakiendelea na zoezi hilo la kutoa hati kwa wateja wanaofika kutia saini zao hati hizo linalofanyika katika ofisi za UTT-PID, jijini Dar es Salaam
opp
Wateja hao wakiendelea kutia saini hati zao katika ofisi za UTT-PID, jijini Dar es Salaam
e
Wateja hao wakipata maelezo ya kina ya kitaaluma kutoka kwa mwanasheria wa UTT-PID, juu ya utiaji saini hati zao hizo za viwanja. zoezi linaloendelea katika ofisi za UTT-PID jijini Dar es Salaam
thumb_DSCN0326_1024.jpgaa
Ofisa wa UTT-PID, Bi. Beatrice akitoa maelezo kwa wateja hao waliofika kutia saini hati zao za viwanja, katika ofisi za UTT-PID, jijini Dar es Salaam hhZoezi hilo likiendelea. Picha ya juu na chini ndani ya ofisi za UTT-PID, jijini Dar es Slaam.
1
Maofisa wa UTT-PID, wakiendelea na zoezi la utoaji wa hati kwa wateja wa viwanja wanaofika kutia saini zao katika ofisi za taasisi hiyo zilizopo jijini Dar es Salaam.

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa