Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba ya uzinduzi rasmi wa Klabu
Zalendo iliyoko katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kwenye Uwanja wa
Ilulu tarehe 10.5.2015. Aliyekaa kushoto kwa Mama Salma ni Mkuu wa
Wilaya ya Lindi Bwana Yahaya Nawanda na kulia ni Mwenyekiti wa Klabu
Zalendo Mwalimu Mwajuma Malugu.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
Na Anna Nkinda – Lindi
Vijana
mkoani Lindi wametakiwa kuwa wazalendo na kutobaguana bali wasambaze
upendo na kujiona wote ni sawa kwa kufanya hivyo wataondoa chuki na
kudumisha amani, mshikamano na umoja katika jamii inayowazunguka.
Mwito huo umetolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akifungua klabu zalendo zilizopo katika Manispaa ya Lindi.
Mama
Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema kama
jamii itajenga tabia ya ubaguzi italeta chuki na upendo utatoweka na
hivyo kusababisha vurugu zitakazopoteza amani iliyopo.
Alisema
uzalendo ni kiini cha maendeleo hivyo huwezi kuwa mzalendo kama hupingi
rushwa na matumizi ya madawa ya kulevya, hutunzi mazingira, hushiriki
kuchangia utoaji wa damu salama na kutokuchangamkia fursa mbalimbali za
maendeleo zilizopo katika jamii yako.
Mama
Kikwete alisema, “Leo hii nimezindua klabu zalendo, Mzalendo ni mtu
mwenye huruma na mtu anayeona thamani ya kitu alichonacho tunzeni vitu
mlivyonavyo ikiwemo Amani ya nchi yetu na mjitoe kufanya kazi kwa bidii
ili muweze kupata maendeleo.
Aidha
Mama Kikwete aliwahimiza wanafunzi kujitendea haki kwa kusoma
kwa bidii hadi elimu ya chuo kikuu kwa kufanya hivyo wataweza kuajiriwa
na kujiajiri katika katika fani mbalimbali na kujiletea maendeleo
katika mkoa wao wa Lindi.
Aliyataja
malengo mengine kuwa ni kuhamasisha wanafunzi na vijana waliopo mtaani
kuwa wazalendo na kuipenda nchi yao kwa kufanya hivyo wataepukana na
mambo yasiyofaa kwa maslai ya nchi yao.
Mwalimu
Mwajuma alizitaja changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni uhaba wa
fedha kwa ajili ya kuandaa makongamao na mabonanza
yatakayosaidia kuimarisha harakati zote za klabu ya uzalendo na
kushindwa kutuma wawakilishi katika mikutano na makongamano ya wanaklabu
ngazi ya taifa.
Pia kikundi kimekosa semina kwa wanaklabu hali inayoplekea wanachama kukosa uelewa wa kutosha kuhusu madhumuni ya klabu hiyo.
Pia
klabu hiyo imehusisha vijana kutoka mtaani wanaofanya kazi za udereva
wa pikipiki maarufu kama bodaboda, wavuvi na wanavikundi vya Sanaa.
Mama
Kikwete aliahidi kukipatia kikundi hicho mipira 20 na jezi seti 10 kwa
ajili ya wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari ambao watashiriki
katika mashindano mbalimbali `na kuangalia utaratibu wa kuwapatia mradi
ambao utawasaidia kuwainua kichumi.
0 comments:
Post a Comment