Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Hatbal Badru mtaalam maabara akiendelea kuwapima afya wananchi mbalimbali wakati wa utoajiwa huduma hiyo.
Kikundi cha waigizaji kikitoa maigizo kama mafunzo kwa wananchi juu ya umuhimu wa huduma za CHF.
Wananchi wakiendelea kupata huduma hiyo
Salvatory Okum Afisa Matekelezo kutoka makao makuu ya NHIF akizizitiza jambo wakati akihamasisha wananchi kujiunga na huduma za Afya ya Jamii CHF
Wananchi wakiendelea kupata huduma hiyo
Abdul Gaucho wa kijiji cha Chumo Uso kwa Uso na Othman Michuzi wa Mtaa kwa Mtaa Blog.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Bw, Rehani Athumani akijadiliana jambo na Mwanaisha Lindu Diwani wa Viti maalum Kilwa wakati alipotembelea na kujionea shughuli za uhamasishaji wananchi wa kijiji cha Chumo kujiunga na huduma ya Afya ya Jamii CHF
Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi Bi. Fortunata Raymond akishiriki kuchezo ngoma ya Wamatumbi wilayani Kilwa.
Wananchi wakiwa wamejipanga kwenye mstari tayari kwa kupima afya zao.
Paul Marenga Afisa Matekelezo mfuko wa Bima ya Afya mkoa wa Lindi akimpima urefu Bi. Mwanaisha Lindu Diwani wa viti maalum wilaya ya Kilwa wakati wa kampeni hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Bw, Rehani Athumani akizungumza na wananchi wakati wa kampeni hiyo iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Chumo.
Mwalimu Chatherine Ngeleja wa shule ya Msingi Chumo kulia na ndugu yake Beata Ngeleja wakisubiri kupata huduma wakati wa kampeni hiyo.
Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi Bi. Fortunata Raymond akihamasisha wananchi kujiunga na huduma ya afya ya jamii CHF wakati wa kampeni hiyo iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Chumo.
0 comments:
Post a Comment