Home » » ZIARA YA KINANA: MWAKYEMBE APEWA SIKU 14

ZIARA YA KINANA: MWAKYEMBE APEWA SIKU 14

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Abdulrahman Kinana, amempa wiki mbili (siku 14), Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, awe ametoa jawabu ni lini wakulima wa korosho na mazao mengine kwenye Mikoa ya Lindi na Mtwara watasafirisha mazao yao kupitia Bandari ya Mtwara.

Bw. Kinana aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi kwenye Uwanja wa Mashujaa Mnarani, mkoani Mtwara na kuongeza kuwa, wakulima hao kutopitisha mazao yao katika

Bandari ya Dar es Salaam ni jambo linayowanyima fursa ya ajira wakazi wa Mtwara pamoja na ushuru.

“Nimempa wiki mbili Waziri Mwakyembe aeleze kwa nini korosho hazipiti Bandari ya Mtwara hivyo kuwanyima fursa za ajira wananchi na halmashauri kukosa ushuru.

“Pia nimemtaka Waziri wa Viwanda na Biashara, aseme ni lini wawekezaji wa gesi watahamia Mtwara na kuweka Makao Makuu yao ili walipe kodi badala ya kukaa Dar es Salaam,” alisema.

Alisema umeme ni tatizo kubwa katika mikoa hiyo; hivyo amemtaka Waziri mwenye dhamana, afike katika mikoa hiyo ili kuwaeleza wananchi ni lini watapata umeme wa uhakika.

Mbunge wa Mtwara, Bw. Hasnein Murji, alisema kitendo cha zao la korosho kushindwa kupitia Bandari ya Mtwara, kinaifanya halmashauri ipoteze sh. bilioni 42 kama ushuru kwa mwaka na kudai Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, ameshindwa kutoa kibali kwa ajili ya ugawaji viwanja.

“Hapa Mtwara tuna mradi wa kupima viwanja 4,000 na fedha za kulipa fidia tunazo, nimekwenda Dodoma kulalamika ili Waziri Mkuu aweze kutupa kibali lakini amekataa,” alisema

Chanzo:Majira

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa