Home » » CRDB YAWASHUKURU WATEJA KUFANIKISHA MAENDELEO

CRDB YAWASHUKURU WATEJA KUFANIKISHA MAENDELEO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

 

BENKI ya CRDB imewashukuru wateja wake kwa kufanikisha kupata maendeleo makubwa, hivyo itaendelea kuwathamini na kuwajali wateja wake.

Akizungumza katika Wiki ya Huduma kwa Wateja, Mkurugenzi wa benki hiyo Charles Kimei, alisema kuwa azma na dira ya CRDB ni kumweka mteja kwanza na kumpa kipaumbele kwa kumsikiliza na kutafuta njia za kutimiza mahitaji yake.

"Benki imekuwa na mpango mkakati wa miaka mitano wa kutoa huduma bora, ubunifu na kuboresha maisha ya wateja wetu na kuwapunguzia gharama za kutufikia," alisema.

Kimei alisema kuwa wiki ya wateja ni wiki muhimu kwao kama benki kwa kuwa inawapa fursa ya kuwatambua na kuthamini mchango wa wateja wao na kupata maoni kutoka kwa wateja.

"Tunapata maoni ni kipi tumefanya vizuri, kipi vibaya na maboresho yanayoweza kufanyika na kuhusisha mambo kadhaa yenye kuonyesha umuhimu wa wateja wetu kwani ndio chanzo cha kila jema linalotokea kwa benki ya CRDB," alisema.

Alisema kuwa mwaka 1996 benki ilianza kutoa huduma kama benki ya biashara ikiwa na matawi 19 tu, rasilimali za bilioni 56, amana za bilioni 40 na idadi ya wateja waliokaribia 100,000.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa hivi sasa benki ya CRDB ni benki inayoongoza nchini Tanzania na kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa taifa na ni kinara wa ubunifu wa maendeleo ya sekta ya fedha nchini.

"Tumeboresha na kubadilisha maisha ya Watanzania wengi kupitia mikopo, kutunza na kukuza amana, kutoa ajira kwa vijana na misaada kwa jamii hadi tumefika hapa tulipo; kwa wateja wetu zaidi ya milioni mbili," alisema.

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa