Home » » CHIZA ATAKA MABORESHO STAKABADHI GHALANI

CHIZA ATAKA MABORESHO STAKABADHI GHALANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza, amesema njia pekee na nzuri ya kumsaidia mkulima ni kuhakikisha  mfumo wa stakabadhi ghalani unaboresha.
Chiza aliyasema hayo juzi kwenye katika siku ya Korosho Tanzania,  iliyofanyika  viwaja vya Ngongo mkoani Lindi.
Alisema kuwa njia nzuri ya kuweza kumsaidia mkulima ni kuhakikisha kwamba taratubu zote zinaboreshwa. 
“Muda mfupi uliopita tu nimejifunza msamiati mpya, nilizoea neno kangomba leo nimesikia chomachoma kwenye ufuta, asubuhi niliuliza mwaka huu sijasikia kelele nyingi za soko la korosho sababu yake kubwa ni nini?
“Nilipata majibu kuwa sababu yake kubwa ni kwamba tulipotangaza bei dira ya korosho, fedha zilipatikana kwa wakati, kwa hiyo mkulima akipata fedha zake hakutakuwepo na migogoro,” alisema.
Waziri Chiza aliongeza kuwa wakulima si kwamba hawaupendi mfumo wa stakabadhi ghalani, isipokuwa hawapendi mambo yanayojitokeza ya ucheleweshaji wa fedha.
“Mimi naamini kuwa mfumo mzima ni mzuri, tunachotakiwa sasa kutafuta yale yote yanayowauzi wakulima katika mfumo huu ili yaboreshwe,”alisema.
 Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Lindi Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa