Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Nape aliyasema hayo katika Kijiji cha Rondo mkoani Lindi juzi, baada 
ya kuulizwa na waandishi wa habari, kwanini baadhi ya wabunge wa CCM, 
akiwemo mbunge wa Newala ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais 
Utawala Bora, George Mkuchika, wanafanya mikutano ya hadhara katika 
majimbo yao wakati serikali ilipiga marufuku mikusanyiko na mikutano ya 
hadhara kwa mikoa ya Lindi na Mtwara.
Nape alisema kuwa sheria ya kutofanya mikutano ilipitishwa na serikali na ni halali na kama mtu anaivunja si sawa, anakiuka.
“Hii sheria ya kutofanya mikutano ilipitishwa na serikali na ni 
halali, sasa kama kuna mtu anaivunja si sawa sawa, kama mnakumbuka hata 
mimi nilivyokuja Mtwara watu wa chama waliniandalia kufungua mashina…Wao
 walidhani kufungua mashina na kuondoka, lakini kwa sababu ya ‘impact’ 
ya Katibu Mwenezi anakuja kikazi, wakaona ingejaza watu na ingevunja 
sheria, waliponiambia tu niliwaambia msifanye mikutano na tulikwenda 
kufanya kikao cha ndani na zile bendera sikwenda kuzipandisha kwenye 
mashina, lakini nikawagawia watu wakaenda kupandisha.
“Uzuri na ubaya wa hii sheria sitaki sana kuingilia ndani kuijadili, 
lakini wakati nilipokuja Mtwara kama mnakumbuka, nilisema kuendelea na 
sheria hii ni kubaka demokrasia, kwa sababu hatuwezi kuzuia watu 
wasifanye shughuli zao za kisiasa kwa muda mrefu kiasi hicho, walizuia 
kwa sababu fulani, kulikuwa na vurugu Mtwara wakati ule juu ya mambo ya 
gesi sasa zimeisha,” alisema.
Chanzo;Tanzania Daima 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment