Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Bodi za mazao nchini zimetakiwa kutatua kero mbalimbali
zinazowakabili wakulima ili kuwajengea uwezo wa kuzalisha kwa wingi na
kufikia mahitaji ya soko la ndani na nje.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Injinia
Christopher Chiza aliyasema hayo wakati akifungua mkutano mkuu wa wadau
wa korosho Tanzania uliyofanyika wilayani Masasi, mkoani Mtwara.
Alisema bodi hizo zinatakiwa kutatua matatizo ya wakulima yanayowakwaza na kushindwa kufikia malengo ya uzalishaji.
Chiza alisema hivi sasa kuna mwanya mkubwa kati ya
bodi, halmashauri za wilaya na miji, mifuko ya pembejeo na wakulima
hali ambayo kimsingi inamuumiza zaidi mkulima.
Waziri huyo alisema sababu ya mwanya huo ni
wakulima kutoshirikishwa katika uamuzi, kama kukokotoa hesabu za
uendeshaji zinazohusu ununuzi, gharama za matumizi na malipo ya majaliwa
ambayo ni kiini cha mafanikio kwa mkulima.
Alisema wakulima wako tayari kuzalisha bidhaa za
mazao, lakini tatizo ni viongozi wa bodi zao kushindwa kutekeleza
matakwa ya wakulima na kutanguliza masilahi yao binafsi.
“Ili mkulima apewe matumaini ya kuzalisha mazao
kwa tija, lazima bodi ziwe mstari wa mbele katika utendaji wa majukumu
yake kwa ufanisi na uaminifu zaidi na kutii sheria ya ushirika na kanuni
za kutamsaidia mkulima,” alisema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho
Tanzania, Anna Abdallah, ameiomba Serikali kuwaajiri watafiti vijana ili
kuchukua nafasi zilizoachwa wazi na watafiti wastaafu.
Alisema mfano kituo cha utafiti cha Naliendele
kilichopo mkoani Mtwara, ambapo kwa sasa kituo hicho kimebaki na mtafiti
mmoja anayefanya kazi kwa mkataba baada ya muda wake wa utumishi kukoma
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment