Mwanamitondo afanyae kazi zake za mitindo nchini Marekani Flaviana Matata, yuko nchini kwa ajili ya kufanya kazi za kijamii kupitia taasisi yake ya Flaviana Matata Foundation. katika mradi wa Back to school project /FMFstationarykit ambao unafadhiliwa na mfuko wa penseni  PSPF,
Baada ya mwezi January Flaviana kugawa vifaa shule za msingi za jijini awamu hii ameenda Mtwara na kufanikiwa kugawa shule  za Msingi  Mtua  na Chemchem ziliyopo Nachingwea  pamoja nashule za msingi Litingi na  Mnengulo ziliyopo Lindi.
bado wanaendelea kugawa vifaa hivyo kwa shule za msingi mikoa mingine "hadi sasa tumeshagawa vifaa kwa watoto 700 na bado kuna kits 800  vitasambazwa Tunduma ,Tunduru na Monduli"
Flaviana alitoa shukran kwa PSPF kwa kudhamini huu mradi na akasisitiza makampuni na mashirika kujaribu kuwezesha elimu kama hali halisi inavyoonekana  kwenye picha hadi leo kuna wanafunzi wanasoma chini na mti, na walio madarasani,madarasa ni mabovu na hayana madawati.
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment